$type=slider$snippet=hide$cate=0

Buyuni kunufaika na REA awamu tatu

Na Issa Ramadhani HATIMAYE kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa nishati ya umeme katika baadhi ya maeneo ya mtaa wa Mgeule, kata ya Buy...

Na Issa Ramadhani

HATIMAYE kilio cha muda mrefu cha ukosefu wa nishati ya umeme katika baadhi ya maeneo ya mtaa wa Mgeule, kata ya Buyuni, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam kimepata ufumbuzi baada ya Shirika la umeme (Tanesco) kuanza kusimika nguzo za umeme kwenye eneo hilo.

Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya mtaa Mgeule, Maliki Shemtandulo(aliyevaa shati la kijani) akifuatiwa na Mjumbe wa baraza la ardhi kata ya buyuni, mtaa wa mgeule, Elizabeth Mwakapangala, wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari wa WM,katika eneo la jengo la ofisi ya mtaa hiyo hivi karibuni (PICHA ETHAN MSUYA

Mwenyekiti wa mtaa huo John Mwatebela, alisema katika mkutano na waandishi wa habari wa taasisi ya habari za vijijini (TTAJA) waliotembelea miradi ya maendeleo katika kata hiyo hivi karibuni kwa lengo la kuandika shughuli za maendeleo pembezoni mwa jiji.

Alisema tayari upembuzi yakinifu umefanywa na shirika hilo kupitia Wakala wake wa Nishati Vijijini (REA) awamu ya tatu ambapo zaidi ya nguzo 80 za umeme zimeanza kusimikwa kwenye maeneo yote ya Mgeule ambayo hayana huduma ya umeme.

"Awamu ya kwanza wakala alianza kazi ya upembuzi kwenye upande mmoja wa eneo la Mgeule maarufu kama Kipawa...baada ya upembuzi walisimika nguzo, kutandaza nyaya na kufanya majaribio ya kuwasha umeme baada ya kufunga transfoma,"alisema.

Kwasasa awamu ya pili inafanyika kwenye sehemu ya Mgeule chini ikihusisha eneo la Mianzini, Kwa Mbogo na Shule ya Msingi Mgeule ambayo pamoja na Kipawa hayana huduma ya nishati ya umeme tangu kuanzishwa kwa mtaa huo miongo kadhaa iliyopita, alisisitiza Mwatebela.

Alisema hadi sasa kazi ya usimikaji wa nguzo na utandazaji wa nyaya umekamilika, na kuongeza kuwa wakati wowote wataweka transfoma na kufanya majaribio ya awali.

Mjumbe wa kamati ya maendeleo ya serikali ya mtaa huo, Maliki Shemtandulo alisema mradi huo ni fursa kwa wakazi wa eneo hilo kibishara kutokana na wengi wao kushindwa kuanzisha biashara zinazotegemea nishati ya umeme licha ya kuwa mtaji na uthubutu.

"Kutokana na kukosekana kwa nishati hii imechangia kwa kiasi kikubwa kushindwa kujiajiri miongoni mwa wakazi ambao wana nia ya kuwa wajasiriamali lakini hawana sehemu za kuhifadhi bidhaa zao kama vile maduka ya dawa zinazohitaji kuhifadhiwa kwenye majokofu (anti biotics), maduka ya nyama na samaki na bidhaa nyingine,"alisema.

Mmoja wa wakazi wa eneo hilo Rashidi Yakub alisema ujio wa nishati hiyo utasaidia katika kutoa nishati kwenye zahanati ya mtaa ambayo inakusudiwa kujengwa kwa nguvu za wananchi baada ya kupata eneo la ujenzi huo.

"Tuliwaza sana namna ya uendeshaji wa huduma za tiba baada ya kukamilika kwa zahanati, lakini tumepata majibu ya hoja hii ya muda mrefu na sasa mioyo yote ni myeupe tunapoelekeza nguvu zetu katika ujenzi huu,"alisema Yakub, Katibu wa Chama cha Mapinduzi tawi la Mgeule `B'.

Mkazi mwingine, Mwanaisha Kibwana alisema ujio wa mradi huo pia utasaidia katika shughuli za soko la mtaa ambalo linakusudiwa kujengwa baada ya mtaa kuanisha eneo la ujenzi huo utakaotekelezwa kwa nguvu za wananchi.

"Pia hata kwenye shule yetu, umeme huu utasaidia kukuza kiwango cha taaluma kwa watoto wetu kwani shule yetu ina madarasa ya kutosha kufungua maabara ya elimu kwa vitendo na pia masomo ya majaribio hata wakati wa usiku, speed test,"alisema Kiwabwana ambaye pia ni Balozi wa shina.


Takwimu zinaonyesha kuwa Serikali kupitia REA awamu ya tatu imeanza utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa nishati ya umeme katika vijiji 12,268 kwenye wilaya zote hapa nchini itakayotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka wa fedha 2016/17 hadi 2020/21.

Waandishi wa habari na viongozi wa mtaa huo,  wakiwa katika moja ya matembezi ya miradi ya maendeleo mtaa wa mgeule  wakiongozwa na  Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya mtaa Mgeule, Maliki Shemtandulo hivi karibuni (PICHA ETHAN MSUYA).


Pia mradi huo utajumuisha vijiji 121 katika maeneo yanayopitiwa na umeme wa msongo wa kilovoti 400 kutoka katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Singida, Tabora na Shinyanga kwa gharama ya dola za Marekani milioni 30 kwa ufadhili wa serikali za Norway na Sweden.

Baadhi ya Transifoma zikifungwa katika moja ya utekelezaji wa mradi REA wa awamu ya tatu
 JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.ttakijiji.blogspot.com ku-install App ya ttajakijiji,  bila ya kuingia websiteTweet@ttajakijijionline, youtube@ttajakijijionline TV, Fb@ttajakijijionline, insta@ttajakijijionline

COMMENTS

Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Buyuni kunufaika na REA awamu tatu
Buyuni kunufaika na REA awamu tatu
https://3.bp.blogspot.com/-JctzhQpWowA/WO9MZhwHqwI/AAAAAAAAAMs/8OiG5ckrS2QLIirjL1Ym2Ar5JSlawDiSACLcB/s640/MG.jpg
https://3.bp.blogspot.com/-JctzhQpWowA/WO9MZhwHqwI/AAAAAAAAAMs/8OiG5ckrS2QLIirjL1Ym2Ar5JSlawDiSACLcB/s72-c/MG.jpg
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2017/04/buyuni-kunufaika-na-rea-awamu-tatu.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2017/04/buyuni-kunufaika-na-rea-awamu-tatu.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy