$type=slider$snippet=hide$cate=0

Diwani Buyuni Lawamani kwa upendeleo

Na  Tatu Mohammed BAADHI  ya wakazi wa mtaa wa Mgeule Kata ya Buyuni katika Manispaa ya Ilala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wamedai...

Na Tatu Mohammed

BAADHI ya wakazi wa mtaa wa Mgeule Kata ya Buyuni katika Manispaa ya Ilala nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, wamedai kukosa huduma muhimu za kijamii kutokana na kukosekana kwa usawa na vipaumbele katika mgawanyo fedha za miradi ya maendeleo za mfuko wa jimbo la Ukonga.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti na timu ya waandishi wa habari wa taasisi ya habari ya Wabunifu (WM) ya jijini humo, wakazi hao wamemlaumu Diwani wa kata hiyo Twaha Malate (CCM) kupendelea baadhi ya maeneo katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa fedha za mfuko huo.


Baadhi ya wajumbe wa Halimashauri kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) tawi la Mgeule kata ya Buyuni, Wilaya ya Ilala wakizungumza na waandishi wa habari wa taasisi ya habari ya Wabunifu (hawamo pichani) walipotembelea miradi ya maendeleo katika eneo hilo hivi karibuni (PICHA: ETHAN MBUYA).

Viongozi wa CCM tawi la Mgeule, Kata ya Buyuni wilaya ya Ilala nje kidogo ya Jiji la Dar es  Salaam wakizungumza na waandishi wa habari kutoka taasisi ya Wabunifu Media hivi karibuni. Kutoka kushoto ni Katibu wa tawi hilo  Rashid Yakub, Lunton William ( Mwenyekiti) na Bruno Benard Ndege, mjumbe wa Halmashauri kuu ya tawi (PICHA: ETHAN MBUYA).
Walisema juhudi zao za kujichangisha kupitia kamati ya maendeleo ya mtaa wamefanikiwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa shule ya msingi bila kuona juhudi za diwani katika kusaidia utekelezwaji wa miradi hiyo kupitia fedha za jimbo.


Tunaishukuru Manispaa na mkoa kwa ujumla wameona juhudi zetu na kuongeza madarasa kutoka darasa moja tulilojenga kwa nguvu zetu na sasa shule ina madarasa 13 na madawati ya kutosha…lakini hatujafaidika na fedha za mfuko wa jimbo tangu diwani achaguliwe,”alisema mmoja, Elizabert Mwakapangala.

Mjumbe wa baraza la ardhi na usuluhishi kata ya Buyuni, Elizabeth Mwakapangala (katikati) ambaye pia ni mkazi wa mtaa wa Mgeule, akizungumza na mwandishi wa habari wa WM, Tatu MohamedKulia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM tawini hapo, Nurdin Shemtandulo.



Waandishi wa habari  wa WM katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa mtaa wa Mgeule. Wa pili kulia ni Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya mtaa huo, Maliki Shemtandulo na wa tatu kulia ni Meneja Miradi wa WM, Moris Lyimo (PICHA: ETHAN MBUYA).

Badala yake fedha nyingi za Kata hiyo kutoka mfuko wa jimbo zimekuwa zikielekezwa zaidi kutekeleza miradi ya maendeleo katika mitaa ya Taliani na Nyeburu kwa kile 
kilichodaiwa kuwa wananchi wa maeneo hayo walimchagua Diwani huyo kwa kura nyingi  na kwamba kitendo cha kuelekeza miradi mingi huko ni kuwapa fadhila.


Waandishi wa habari wa WM  wakiwa kwenye eneo la ujenzi wa zahanati ya mtaa huo ambapo pia walishuhudia kituo cha mama na mtoto (PICHA: ETHAN MBUYA).
Mjumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Mtaa wa Mgeule, Kata ya Buyuni Manispaa ya  Ilala, Maliki Shemtandulo akionyesha waandishi wa habari wa WM mojawapo ya sehemu ulipojengwa shule ya msingi Mgeule walipotembelea shuleni hapo hivi karibuni (PICHA: ETHAN MBUYA).
Meneja Miradi wa WM na Mwenyekiti Mtendaji wa TTAJA, Moris Lyimo  (aliyesimama katikati) akifafanua jambo kwa wafanyakazi wenzake kabla ya kuanza kwa  ziara ya kutembelea miradi ya maendeleo katika mtaa wa Mgeule, Kata ya Buyuni, Manispaa ya Ilala Jijini Dar es Salaam hivi karibuni  (PICHA: ETHAN MBUYA).

Mwananchi mwingine, Baraka Koka alisema eneo hilo lina kila sababu ya kupewa kipaumbele kutika fedha za mfumo wa jimbo kutokana na adha ya mafuriko wakati wa msimu wa mvua kwa kukosa daraja na kusababisha mahudhurio yasiyoridhisha kwa wanafunzi na shughuli nyingine za kijamii.

“Hapa kwetu kuna mabonde yanayoweza kuvukika msimu wa mvua kwa kujenga madaraja tu, fedha za jimbo zinatolewa kwenye kata lakini hatuoni kipaumbele hiki kikitekelezwa japokuwa ni huduma mtambuka,”alisema Koka.
Baadhi ya majengo ya shule ya msingi Mgeule ambayo sehemu yake imejengwa kwa nguvu za wananchi wa mtaa huo, uliopo kata ya Buyuni, Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam. Kwa sasa shule hii iliyojengwa kwa muda wa mwaka mmoja ina wanafunzi zaidi ya 700 (PICHA: ETHAN MBUYA).









Sehemu ya wananchi wa mtaa wa Mgeule katika mkutano na waandishi wa habari wa WM walipotembelea mtaa huo hivi karibuni (PICHA: ETHAN MBUYA).

Naye Mwenyekiti wa mtaa huo, John Lazaro Mwatebela alisema kuwa juhudi za pamoja zinahitajika katika kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuangalia vipaumbele kulingana na ukubwa wa kero katika dhana ya kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu ya `Hapa Kazi Tu’.

Alikiri eneo hilo kukabiliwa na kero kadhaa ingawa baadhi zimepunguzwa kwa juhudi binafsi, nguvu za wananchi na Manispaa.


 “Tunashukuru juhudi za serikali hasa Manispaa ya Ilala kwa kuuunga mkono juhudi zinazoanzishwa na wananchi, ingawa nguvu ya serikali inahitajika zaidi katika kutatua kero nyingine ufumbuzi wake umeanza kwa sisi kubuni namna ya kukabiliana nazo,”alisema.

Kwa upande Diwani Malate alikanusha tuhuma hizo kwa madai kuwa amehusika katika ujenzi wa shule moja kwenye mtaa huo kwa idadi ya madarasa nane.


"Madai yao sio ya kweli. Huo mtaa wa Nyeburu wanaousema sijafanya chochote, ila kinachofanyika pale ni kwamba Mwenyekiti wa mtaa huo (Nyeburu) anatumia pesa zake mwenyewe sasa watu wakiona tingatinga linachonga barabara wanajua mimi ndiye ninafanya," alisema na kuongeza …
"Wananchi kulalamika ni haki yao kwani kata yangu ina mitaa 8 ni kubwa mno, sijawahi kupata mradi hata mmoja... bajeti ni ndogo ingawa naendelea kufatilia, ninawaomba wawe na subra, hakuna kero ambayo haitatatuliwa," alisema Malate.
=================


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.ttakijiji.blogspot.com ku-install App ya ttajakijiji,  bila ya kuingia websiteTweet@ttajakijijionline, youtube@ttajakijijionline TV, Fb@ttajakijijionline, insta@ttajakijijionline

COMMENTS

Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Diwani Buyuni Lawamani kwa upendeleo
Diwani Buyuni Lawamani kwa upendeleo
https://2.bp.blogspot.com/-VXntp01J9KE/WNtvIHtMkUI/AAAAAAAACOY/f6c2Bf3SetguoaBgiGqb9Noq5m36tB_nQCLcB/s640/DSC_0074.JPG
https://2.bp.blogspot.com/-VXntp01J9KE/WNtvIHtMkUI/AAAAAAAACOY/f6c2Bf3SetguoaBgiGqb9Noq5m36tB_nQCLcB/s72-c/DSC_0074.JPG
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2017/03/diwani-buyuni-lawani-kwa-upendeleo.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2017/03/diwani-buyuni-lawani-kwa-upendeleo.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy