$type=slider$snippet=hide$cate=0

Nassira: Ninafanya makubwa kwa biashara ya kuni, sambusa

Nassira: Ninafanya makubwa kwa biashara ya kuni, sambusa Caption:   Nasra Selemani akiwa kwenye kibanda chake cha biashara ya kun...



Nassira: Ninafanya makubwa kwa biashara ya kuni, sambusa

Caption:  Nasra Selemani akiwa kwenye kibanda chake cha biashara ya kuni katika soko la Kiwalani jijini Dar es Salaam, 

Na Yasmine Protace

KATIKA miaka ya hivi karibuni kumekuwa na mwamko kwa baadhi ya watu hasa wanawake kufanya biashara ya kuuza kuni na kuwa kichocheo kimojawapo cha maendeleo katika ngazi ya kaya hapa nchini.
Tofauti na maeneo mengi, biashara ya kuuza kuni imeshamiri kwa wingi jijini Dar es Salaam kutokana pia na mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo inayotumika kama nishati ambayo inaaminika haitumii gharama kubwa ukilinganisha na mkaa, umeme, gesi na nishati nyingine mbadala.

Biashara ya kuni jijini humo imekuwa ikifanyika kwenye masoko, kwa mfano soko la kimataifa la samaki la lililopo eneo la Magogoni ambako wafanyabiashara wa samaki wamekuwa wakinunua kuni kwa ajili ya kukaangaa samaki, na masoko mengine makubwa  kwa ajili ya kupikia. Baba na Mama lishe kwenye masoko hayo ndiyo wateja wakuu.
Kwa takriban miaka mitatu sasa, Nassira Selemani amekuwa mfanyabiashara wa kuni katika soko la Kiwalani, Ilala jijini humo iliyotokana na biashara ya kuuza sambusa kwa  mtaji wa Shilingi 15,000.
Mtaji huo anasema alipewa na dada yake Januari 2013 baada ya yeye (Nassira) kukaa nyumbani kwa muda mrefu bila shughuli ya kufanya jambo ambalo anasema kwa familia alionekana kama kero, ndipo dada yake huyo alipofikia uamuzi wa kumpatia mtaji.
“Kwa kweli ilikuwa ni fedha ndogo sana, kiasi kwamba niliwaza sana ni kwa namna gani fedha hizo nitaziendesha…lakini dada alinipa maarifa na kunitia moyo wa kuanza kidogokidogo kupika sambusa za viazi vutupu,”anasema. 
Anasema baada ya kumuelewa dada yake alitumia mtaji huo kununua viazi mbatata (ulaya) kiasi cha kilo mbili, ngano kilo mbili, mafuta lita moja na mkaa makopo mawili. Alianza kutengeneza sambusa 150 hadi 200 na kuziuza mtaani kwa kila sambusa Sh.100 ambapo kila siku alifanikiwa kukusanya Sh.15,000 hadi 20,000.
“Wateja wangu wengi walikuwa ni watoto na hasa wanafunzi. Mauzo yalipanda na kushuka, kuna siku sambusa zinanunuliwa zote, kuna siku nyingine hali inakuwa mbaya napata 10,000 au chini ya hapo,”anasema.
Anasema aliendelea na biashara yake hiyo huku akitafuta mbinu za upishi wa kisasa na mbinu zaidi za kibiashara, ambapo siku moja akiwa katika soko la Kiwalani kununua malighafi alifanikiwa kukutana na wataalamu wa Shirika la Eguality For Growth (eFG) wakiwa wamewatembelea akina mama wanaofanya biashara sokoni hapo na kuwaleza hitaji lake hilo la elimu ya ujasiriamali.
Anasema juni 2013 eFG walifika tena sokoni hapo kufundisha elimu ya kuweka na kukopa kwa njia ya vikundi (vikoba) naye kuwa mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.
Mbali ya kujifunza mbinu za kibiashara, aliweza kutambua umuhimu wa kuweka akiba baada ya kupata mifano mbalimbali kupitia mafunzo hayo ya wanawake waliofanikiwa kwa kiwango cha juu baada ya elimu hiyo.
Anasema aliamua kumega sehemu ya mtaji wake na kuanza kuwekeza kwa kununua hisa katika kikundi cha kimoja cha kikoba kwa kuanza kununua hisa tano kwa kila hisa moja  Shilingi 10,000, alifanya hivyo kwa kipindi cha miezi sita mfululizo bila kukopa.
Mwaka 2014 aliweza kukopa 700,000/-na kufanikiwa kuongeza mtaji wake kufikia  zaidi ya laki tisa.
“Nilijaribu kutafuta ushauri kwa watu mbalimbali akiwamo dada yangu aliyenipa mtaji wa awali, ili ikiwezekana nianzishe biashara nyingine. Katika mazungumzo hayo nilipata ushauri wa kuanza biashara ya kuuza kuni na kuanza kufanyia kazi ushauri huo,”anasema.
Anasema hakukurupuka kuanza biashara hiyo, alichofanya ni kutafuta masoko, ambapo mwana kikoba mwenzake alimweleza kuwa anaweza kujaribu biashara hiyo katika soko la Kiwalani kutokana na sokoni hapo kuwa na uhitaji mkubwa wa kuni kwa idadi kubwa ya watumiaji hasa wapishi.
Anasema Desemba 2014 alifika sokoni hapo na kukutana na uongozi wa soko na kukubaliwa kuanza biashara baada ya kupatiwa kizimba.
Anasema fedha zote alizokopa alizitumia kama mtaji wa kuanza biashara ya kuni na kuachana na biashara ya awali ya kuuza sambusa.
“Nilikwenda idara ya misitu (maliasili) kujua taratibu, ambapo nilitakiwa kulipia kibali 150,000/- na kusafiri hadi Chole, mkoani Pwani ambako kuna misitu. Nilifanikiwa kupata mzigo na kuusafirisha hadi sokoni Kiwalani kwa malipo ya usafiri Sh.150, 000,”anasema.
Wateja wake wakubwa ni wafanyabiashara wanaokaanga na kuuza samaki ambapo mzigo mmoja wa kuni huuza 1,000/-.
''Kuni zina faida kubwa zaidi, kila baada ya wiki  tatu ninakwenda kuchukua mzigo mwingine…hizo laki saba hivi sasa zimejizalisha na mtaji wangu umeongezeka na kufikia zaidi ya milioni moja,”anasema.
Faida anazopata kwa kuendesha biashara hiyo ni kwamba ameweza kujitegemea mwenyewe kwa kuhama kwa dada yake na ameweza kupanga nyumba ya vyumba viwili ambapo kwa mwaka analipa kiasi cha shilingi 720,000.
Anasema pia biashara ya kuuza kuni imemsaidia kuboresha maisha yake ikiwamo kuwalipia watoto wake ada katika shule za serikali.
Anazungumzia malengo yake, anasema mpango wake ni kutanua wigo katika biashara yake ikiwamo kufungua biashara nyingine ambazo hajaziainisha kwa maelezo kuwa anaendelea kukusanya mtaji na utafiti wa masoko.
Kuhusu changamoto, anasema mojawapo ni kutofautiana na polisi wanapokutana barabarani kwa kuwasumbua huku akiwa amefuata taratibu zote za vibali.
''Ninalipia mzigo na nina vibali vyote vya maliasili, lakini jambo la kushangaza na kusikitisha sana  ni pale unapokutana na polisi, wanakusimamisha bila sababu ya msingi hata ikiwaonyesha kibali hawakuelewi, ingawa baada ya kusumbuana sana wanakuachia, hata hivyo unakuwa umepoteza muda mwingi bila sababu,''anasema.
Changamoto nyingine ni baadhi ya wanunuzi kutokuwa waaminifu, ambapo huamua kujiongezea kuni kutoka wastani uliowekwa na kusababisha hasara.
Tatizo lingine ni ukatili wa kijinsia ambapo baadhi ya wanaume wamekuwa wakiwadhalilisha wanawake kwa lugha za matusi, kejeli na maneno yasiyofaa.
Hata hivyo amesema kwa msaada ( eFG) hali hiyo imetoweka sokoni hapo baada ya shirika hilo kutoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia na madhara yanayoweza kumpata mtu anakuwa chanzo cha tatizo hilo.
Elimu nyingine ambayo imewasababisha wafanyabiashara kuwa na upeo na kuacha masuala yasiyokuwa na tija na mzaha ni namna ya kuandaa vikoba na jinsi ya kunufaika navyo na wanawake kugombea nafasi mbalimbali uongozi sokoni hapo ambapo kwa sasa wafanyabiashara wengi wako makini  katika masuala ya msingi.
Anasema pia analishukuru shirika lisilokuwa la kiserikali la Legal For Service (LFS) kwa kuandaa mradi wa mjaribio wa mwaka mmoja katika baadhi ya masoko, na kuvishirikisha vyombo vya habari kuwa pamoja na wafanyabiashara kwa ajili ya kufanya kazi kwa pamoja.
"Huu mradi ni mzuri tumeweza kuwa karibu na vyombo vya habari na tunafanya kazi pamoja, hii imetupa sana faraja wafanyabiashara kujua matatizo yetu sehemu ya kuyapeleka na  hali hiyo itasaidia kuyafanyia kazi,''anasema.
Pia aliwataka wakina mama wasiokuwa na shughuli za kufanya kutobweteka nyumbani wakiwategemea waume zao badala yake wawe na utamaduni wa kujishughulisha katika biashara ndogondogo ili waweze kupata mikopo ambayo itawasaidia katika kujikwamua katika maisha ya baadaye.
"Kuna baadhi ya akina mama hawataki kujishughulisha na biashara zozote kwa madai kwamba waume zao wana vipato, lakini wajue siku inaweza ikabadilika wakajakujutia muda waliokuwa wakikaa nyumbani bila ya kujishughulisha wanajilaumu baada ya kuachwa, kwani hilo linawezekana pia likawapata,''anasema.
Elimu ya mashirika yasiyokuwa ya kiserikali ni muhimu kwa wafanyabiashara ambao pamoja na kupata fedha katika biashara zao, hata hivyo ukosefu wa elimu ya biashara imekuwa kikwazo katika uendeshaji wa shughuli zao na kujikuta wakiwa `watumwa’ katika ukopaji.
Utafiti unaonyesha kuwa wanawake wengi ni hodari kukopa mikopo midogo midogo kwenye taasisi za fedha kama vile FINCA, PRIDE na benki bila kuwa na elimu ya namna ya kusimamia mikopo au miradi na biashara vinavyoendeshwa kwa kutumia fedha za mikopo kama hiyo.
Hata hivyo, mradi wa uelimishaji wanawake na wafanyabiashara wengine kwenye masoko jijini Dar es Salaam chini ya LFS na eGF imetajwa kuleta mabadiliko makubwa kwa makundi hayo kutambua fursa zao na namna ya kuzitumia kujiletea maendeleo.
=======
Imetumika TAIFA LETU

COMMENTS

Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Nassira: Ninafanya makubwa kwa biashara ya kuni, sambusa
Nassira: Ninafanya makubwa kwa biashara ya kuni, sambusa
http://4.bp.blogspot.com/-2qCfxgP2RbY/VqifrF34xKI/AAAAAAAAAK4/nBAVp530aws/s400/picha%2Bb.JPG
http://4.bp.blogspot.com/-2qCfxgP2RbY/VqifrF34xKI/AAAAAAAAAK4/nBAVp530aws/s72-c/picha%2Bb.JPG
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2016/01/nassira-ninafanya-makubwa-kwa-biashara.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2016/01/nassira-ninafanya-makubwa-kwa-biashara.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy