$type=slider$snippet=hide$cate=0

Rabika: Shamba la ufugaji kuku mfano wa kuigwa kwa ajira, mafunzo

  Sehemu ya kuku wa aina mchanganyiko, RHODE ISLAND RED na  KUROILER wanaofugwa katika shamba la mradi wa RABIKA POULTRY FARM Kata ya...



 
Sehemu ya kuku wa aina mchanganyiko, RHODE ISLAND RED na  KUROILER wanaofugwa katika shamba la mradi wa RABIKA POULTRY FARM Kata ya Kibamba, Wilaya ya Mkuranga Mkoa wa Pwani (Picha TTAJA).

Na Komba Kakoa na Eligius Nyoni


“NI kijiji katikati ya pori, lakini wanyama wake ni kuku. Tofauti yake ni kwamba majengo yake yameezekwa kwa mabati, tena kwa unadhifu mkubwa sana. Tunaposogea zaidi, tunakaa kwenye nyumba ya msonge, macho yanaanza kupepesa huku na kule,
pamependeza mno, ni kijani kibichi, mmoja wetu anasimama na kutupa macho mbali na kuibuka na maneno, he! Kumbe hii ni ranchi ya kuku, wengine tukaangua kicheko,” ni kauli ya mmoja wa wajumbe wa timu ya waandishi wa habari  wa chama cha waandishi wa habari za vijijini (TTAJA) waliotembelea shamba la ufugaji kuku, kikiji cha Rabika, Kata ya Kibamba wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani.

“Msisitizo mkubwa unaowekwa na serikali ni watu kuwa na mawazo ya kujiajiri, tupo ambao tumeanza kuthubutu kwakutambua kwamba serikali haina uwezo wa kuajiri kila mtu, jambo la kustaajabu ni pale wale tulioanza kuthubutu tunakosa ushirikiano kutoka kwenye mamlaka serikalini,” hiyo pia ni kauli ya Hamid Abdullkarim, meneja wa shamba hilo akifungua pazia la ziara hiyo.
Abdullkarimu, anasema pamoja na changamoto hiyo mpango wao ni kuongeza uzalishaji na masoko, kupanua mradi kwa kuanzisha shamba jipya na vitendea kazi muhimu ili kufikia malengo ambayo kiasi fulani wameanza kuyachungulia.
Meneja huyo aliiambia timu ya waandishi wa habari wa chama cha waandishi wa habari za vijiji cha Tanzania Transparency Journalists Association (TTAJA) waliotembelea mradi huo Agosti 21 mwaka huu kuwa walianza mradi huo baada ya kufanya utafiti wa aina za kuku wanaomudu mazingira yote na pia kulingana na soko.
“Tulifanya utafiti wa awali mwaka 2009 kabla ya kuanza kwa mradi mwaka 2010.Utafiti ulijumuisha aina za kuku kwenye mataifa mengine ya nje ambao wakichanganywa wanaweza kuuzika katika soko la ndani na nje,”anasema.
Meneja wa shamba la Rabika Poultry Ahmed Abdullkarim
Anasema utafiti huo ulionyesha kuwa aina bora ya ufugaji  wa kuku ni ile ya Nusu Huria ambayo uzalishaji licha kutumia gharama nafuu, inastahimili magonjwa, kuku kuishi kwenye mazingira ya aina zote ulinganisha na aina ya kisasa zaidi (Commercial broiler) ambayo pamoja na kutumia gharama kubwa, nyama ya kuku wa aina hiyo imekuwa na changamoto nyingi, ikiwamo walaji kukimbia nyama yake kwa kuhofia kemikali zinazotumika katika uzalishaji.
Ufugaji huria katika shamba hilo linalotambulika kama Rabika Poutry Farm hujumuisha aina ya kuku wanaotambulika kitaalamu kama New Hamshire wenye rangi nyekundu  kutoka nchini Burundi wenye asili ya Uingereza.
Anasema aina hiyo hutumika kwa ajili ya nyama na mayai wenye uwezo wa kukua kwa uzito wa  kilogramu 2 hadi 4, hutaga mayai kuanzia 140 hadi 200 kwa mwaka.
Aina nyingine ni Rhode Island Red pia wa rangi nyekundu ambao uzalishaji wake ulianzia nchini Uholanzi mwaka 1961. Aina hiyo hukua na kufikia wastani wa kilo 2 hadi 2.5 na hutaga mayai 200 hadi 250 kwa mwaka na yana uzito wa gramu 45 hadi 100 kwa mwaka.
Anazitaja aina nyingine kuwa ni Kuroiler zenye rangi mchanganyiko kutoka Uganda wenye asili ya India ambao hufugwa kwa ajili ya nyama na mayai, hutaga mayai kati ya 150 hadi 250 yenye ukubwa wa gramu 45 hadi 80. Aina hiyo ya kuku hunenepa na kufikia kilo 2 hadi 4.
Pia wanafuga kuku aina ya Black Austrolop (wenye rangi nyeusi) kutoka nchini Malawi ambao hufugwa kwa ajili ya mayai, hutaga mayai kati ya 200 hadi 250 kwa mwaka yakiwa na ukubwa wa gramu 45 hadi 75.

MAFANIKIO:

Meneja huyo wa Shamba la Rabika anasema wakati wanaanza mradi huo mwaka 2010 walianza kwa mtaji mdogo wa kufuga wazazi (Parent stock)  kuanzia ngazi ya vifaranga 300 ambapo waliweza kuwakuza na kufikia kiwango cha kutaga.
Waliweza kuongeza uzalishaji huo mara dufu kwa kiwango cha wazazi 600 na kutumia mafanikio hayo kununua mashine za utotoleshaji wa vifaranga kwa mayai waliyokuwa wanazalisha kupitia idadi hiyo ya wazazi.
“Baada ya kununua mashine za utotoleshaji tulifanikiwa kuongeza zaidi mazao na kufikia kuku 1,236 kwa kipindi kifupi sana…ongezeko hilo lilitutia faraja, ambapo tuliongeza kuku 800 zaidi na kufikia idadi ya  kuku 2,000 wa aina tofauti tofauti,”anasema Abdullkarim.
Anasema ufugaji wa kuku kwa mfumo wa Nusu Huria, huzingatia kanuni za kitaalamu na maelekezo mengine una tija katika soko la ndani na nyama, na kushauri jamii kuhama kwenye mfumo huria ambao kuku wengi hudumaa kutokana na kukosa lishe sahihi na magonjwa.
Kwa hali hiyo, jamii ya wakulima wamekuwa wakifuga kwa mfumo ambao hauna tija jambo ambalo husababisha jamii husika kutofikia malengo ya ufugaji, anasema.
Anasema sehemu kubwa ya wakulima na jamii nyingine barani Afrika zimeachana na ufugaji huria wa kuku na kujiunga na mfumo wa nusu huria akitolea mfano wa nchi kadhaa kama vile Malawi, Uganda, Burundi na Rwanda kwa kusema kuwa zimepiga hatua kubwa kimaendeleo kupitia nyama ya kuku baada ya kujiunga na mfumo wa nusu huria.
Ufugaji kuku wa Nusu Huria umekuwa na mafanikio makubwa kwa wao wa kuku wa kuku kwa mtindo wa nusu huria, ni mfumo ambao mfugaji hutumia mbinu za kitaalamu katika ulishaji kwa mfumo usiotofautiana sana na ule wa huria. Kuku wanaofugwa katika mfumo huo huwekwa kwenye kizuizi kama ilivyo mfumo wa kisasa ingawa hutofautiana kidogo na mfumo kisasa (broiler) ambao wakati wote kuku huhifadhiwa bandani. Mfumo wa Nusu Huria huwawezesha kuku kuishi kwa kula na kutoka nje ya mabanda kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa nyavu jambo ambalo kwa mazingira ya kuku wa kisasa (broiler) siyo rahisi kuishi.
Pia mfumo wa Nusu Huria kuku huweza kuwa mabandani wakati wa kulala (usiku) baada ya kuwa nje ya mabanda kwenye eneo maalumu lililotengwa kipindi chote cha mchana. Pia uzalishaji wa Nusu Huria hutofautiana kidogo na mfumo wa kuku wa Broiler.
“Tumefanikiwa kutoa ajira kwa vijana sita ambao tunasaidiana nao katika kuhudumia mifugo yetu kila siku kwa chakula na dawa na kuhakikisha mradi wetu unaimarika,”anasema.

MIPANGO YA BAADAYE:

Anasema pamoja na changamoto zilizopo, mpango wao ni kuongeza uzalishaji zaidi, kuwa na mashine yao wenyewe  ya kuzalisha chakula cha kuku badala ya kununua chakula kwenye maduka ya vyakula vya kuku ambacho hatuna uhakika nacho kutokana na wazalishaji wasiokuwa waaminifu.
“Tayari tumejenga kituo cha uzalishaji…hivi sasa tupo kwenye mchakato wa kuweka mashine ya kusindika chakula ili tuachane na kununua chakula ambacho hatuna uhakika na utengenezwaji wake, ambao mara nyingi umekuwa ukitutia hasara tukiamini kina virutubisho, kumbe kimechakachuliwa… ni kuhatarisha afya ya kuku,”anasema.
Anasema wamewasiliana na uongozi wa wilaya kwa ajili ya kufikisha ombi kwa wakala wa nishati ya umeme vijijini (REA) ili kufungiwa umeme ambao umeishia kijiji cha Kibamba, kilometa tatu kutoka kijiji cha Rabika ulipo mradi huo.
Anasema uongozi mzima wa Wilaya hiyo uliwahi kuongozana na Mwenge wa Uhuru  na kufika kwenye mradi huo na kufanikiwa kufungua jengo la utawala la shamba hilo, ambapo viongozi mbalimbali akiwamo Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga waliahidi kushirikiana nao kwa lengo ka kuondoa changamoto zinazowakabili, ikiwamo tatizo hilo la umeme.
Anasema Mkuu wa wilaya hiyo amekuwa akiwatembelea mara kwa mara, kuwapongeza na kuwaahidi kushirikiana nao, kuhamasisha jamii kwenda kufika kwenye shamba hilo na kujifunza mbinu za ujasiriamali ambapo yeye mwenye (Mkuu wa Wilaya) amechukua vifaranga ili kuanza ujasiriamali huo kama mfumo kwa wanajamii wengine.
Mipango mingine ni pamoja na kuongeza mtaji  wa Shilingi milioni 200 kutoka mtaji wa sasa wa milioni 100  ili kufikia malengo ya hitaji la  mtaji uwekezaji wa Sh.miilioni 300 kufikia malengo ya uzalishaji zaidi katika shamba jipya la  ekari 50 huko kijiji cha Kisegese, na shamba la sasa litatumika kama kituo cha usambazaji na majaribio.
Pia aliwaambia waandishi hao wa TTAJA kuwa mipango yao mingine ambayo utekelezaji wake unaanza mwaka 2016 ni pamoja na kuwa na mashine za kunyonyoa, kuongeza uzalishaji wa nyama ya kuku tani 5 hadi 10 kwa siku, kuwa na gari lenye deep freezer (storage van), mashine za kufungashia, duka la nyama, kuongeza kuku (wazazi) kufikia 5,000 kutoka wastani wa sasa wa wazazi 2000 na kuongeza uzalishaji wa mayai kutoka trai 15 kwa siku sasa.

CHANGAMOTO:
Changamoto mojawapo ni hitaji kubwa la nyama ya kuku wa ufugaji wa  nusu huria ukilinganisha na kiwango cha nyama inayozalishwa. Anasema kwa sasa wateja wao wakubwa ni wafugaji wadogo ambao wamekuwa wakifika kituoni hapo na kufundishwa mbinu mbalimbali za ufugaji, ingawa mpango wao ni kuwafikia wafugaji wakubwa, hoteli kubwa za kisasa kwa ajili ya nyama.
Changamoto ushirikiano mdogo kati yao na baadhi ya viongozi kwenye idara za serikali kwa maelezo kuwa kumekuwa na ukiritimba pindi wanapofika kwa ajili ya kutafuta ushauri wa kitaalamu.
“Tumekwenda pale wizarani, lakini kila wakati ni kusumbuliwa…katika halmashauri pia wapo maofisa ugani lakini hata mmoja sijawahi kumuona amefika hapa na kututembelea ili kuona juhudi zetu katika kuisaidia serikali kutoa ajira…mambo haya hayapendezi hata kidogo,”anasema Abdullkarim.
Kwa upande wake meneja wa Utawala na Masoko wa mradi huo, Zahor Zahor anasema tatizo la hawa watafiti wa kuku  hapa nchini ni tatizo.
“Hili ni tatizo kubwa, ni lazima serikali yetu izinduke sasa na ione umuhimu wa sekta ya kuku katika kuchangia ajira kwa kuwabaini watafiti wa kuku na kuwatumia…kwa kufanya hivyo ni lazima sekta hii itakuwa kwa haraka na bila shaka kutakuwa na ushindani sawa wa soko la nyama kama ilivyo kwenye nchi nyingine,”anasema Zahor.
Naye mfanyakazi mkuu wa shamba hilo, Magambo Fanuel anasema kumekuwa na mafanikio makubwa kwa vijana wanaozunguka mradi huo, licha ya baadhi yao kutopenda kujishughulisha hasa kwa shughuli za maeneo ya vijijini.
Fanuel anasema vijana wengi wametembelewa na uongozi wa mradi na kuelezwa manufaa ikiwa watafika na kufundishwa mbinu za ufugaji kwa maisha yao ya baadaye, hata hivyo ni vijana wanne waliofika na kufundishwa ingawa kijiji hicho na kile cha jirani cha Kibamba kina vijana wengi.
“Hii inasikitisha sana, vijana wanatakiwa kutambua kwamba siyo wakati tena wa kuchagua kazi…naaamini kwamba kama wangejitokeza kwa wingi wakafika hapa wangepatiwa mafunzo…kisha wakapatiwa vifaranga vya kuanzia ni lazima watabadilika kiuchumi na kujipatia ajira,”anasema.
Msimamizi huyo wa shamba anasema: “Hiki sio kipindi cha vijana kutegemea ajira kutoka serikalini ila wanapaswa kuthubutu na kuhakikisha wanajituma kwa bidii ili waweze kujikwamua katika wimbi la umasikini,” anaongeza.
Anasema amepata manufaa makubwa tangu ajiunge na mradi huo mwaka jana ambapo ameweza kusomesha watoto wake, mmoja shule ya sekondari Makongoro na mmoja shule ya Msingi Busore, wilayani Bunda mkoa wa Mara.

COMMENTS

BLOGGER: 1
Loading...
Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Rabika: Shamba la ufugaji kuku mfano wa kuigwa kwa ajira, mafunzo
Rabika: Shamba la ufugaji kuku mfano wa kuigwa kwa ajira, mafunzo
http://2.bp.blogspot.com/-ZJ9_kdW06_A/VeA7AixOVtI/AAAAAAAAAFQ/gzwaZSJvN-w/s400/Rhode%2BIsland%2BRed.JPG
http://2.bp.blogspot.com/-ZJ9_kdW06_A/VeA7AixOVtI/AAAAAAAAAFQ/gzwaZSJvN-w/s72-c/Rhode%2BIsland%2BRed.JPG
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2015/08/rabika-shamba-la-ufugaji-kuku-mfano-wa.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2015/08/rabika-shamba-la-ufugaji-kuku-mfano-wa.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy