Na Komba Kakoa IMEELEZWA kuwa utitiri wa wanafunzi katika madarasa umekuwa ukichangia kushusha kiwango cha ubora wa elimu inay...
Na
Komba Kakoa
IMEELEZWA
kuwa utitiri wa wanafunzi katika madarasa umekuwa ukichangia kushusha kiwango cha ubora wa elimu
inayotolewa kwa wanafunzi wa msingi na sekondari hapa nchini.
Hili
linatokana na ukweli kwamba madarasa yenye msongamano wa wanafunzi yamekuwa
mzigo mkubwa kwa walimu wanapofundisha
hali inayowafanya kushindwa kueleweka kwa wanafunzi wote kwa wakati
mmoja.
Mbali
na hiyo, mwalimu anayefundisha katika madarasa yenye wanafunzi wengi imampa
wakati mgumu kuweza kujua tabia za kila mwanafunzi na hasa pale anapotaka
kupima maendeleo ya mwanafunzi mmojammoja.
Kutokana
na hali hiyo wadau wa maswala ya elimu wanasema kwamba madarasa yenye
msongamano wa wanafunzi yanachangia walimu kushindwa kutekeleza vizuri malengo
yao ya kutoa elimu kwa vitendo.
Wanafunzi wakiwa wamejazana darasani huku wengine wakikaa chini kutokana na ukosefu wa madawati hali ambayo inaathiri uelewa wa mwanafunzi pamoja na ufundishaji wa mwalimu. |
Kadhalika
wadau hao wanasema kuwa mwalimu anayefundisha katika madarasa ya aina hiyo anatumia muda mwingi katika
kufundisha somo lake na kuhakikisha kila mwanafunzi anayehudhuria kipindi chake
ameelewa.
Stephen
Kika, ni mwalimu wa shule ya Msingi Mgambo, iliyo katika wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga anasema hali hii
husababisha mwalimu kushindwa kudhibiti wanafunzi wake.
Kika
ambaye pia ni mwalimu wa Taaluma katika shule hiyo anasema kutokana na uwepo wa
idadi kubwa ya wanafunzi katika chumba cha darasa humwia ngumu mwalimu kubaini
tabia za wanafunzi wote hasa walioketi viti vya nyuma au walio kosa
kabisa,”nasema Mwl. Kika.
“Madarasa
ya aina hii yanahitaji jitihada kubwa ya mwalimu katika kudhibiti muda wa
ufundishaji, kwasababu humlazimu mwalimu kutumia muda mwingi katika kufundisha mada moja,”Anasema Mwl.
Kika.
Kwa
upande wake Mwalimu Aisha Hemed, ambaye pia ni mwalimu anasema idadi kubwa ya
wanafunzi na ukubwa wa madarasa, huwakosesha walimu wasiweze kuwa na ari pamoja na nguvu ya kufundisha.
Mwl.
Aisha ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la Kiserikali la Youth for
Development (Y4D) anasema kuwa hali hiyo haimuathiri mwalimu pekee bali
huathiri tabia na usomaji wa mwanafunzi pia kwa kumfanya asijishughulishe zaidi
katika masomo na shughuli za kijamii kwa ujumla.
Mwl.
Aisha anasema kuwa katika ufundishaji, usikivu wa wanafunzi darasani ni jambo
la muhimu linalopaswa kupewa kipaumbele kutokana na ukweli usiopingika kwamba
unaathiri ushiriki wake katika masomo.
“Utafiti
unaonyesha kuwa madarasa yenye watu wachache wanafunzi wanatumia muda mchache
kufanya mazoezi yao na yanatoa nafasi kufanya mazoezi mengi zaidi pia wana
uwezo wa walimu hupata fursa ya kuwa karibu na watoto wote na kuwafanya
wawajibike kuliko kuwadharau wanafunzi
wenye uwezo mdogo kiakili darasani.
Hata
hivyo Mwl. Aisha anaukosoa mfumo uliopo kwamba kumekuwa na tabia ya ujengaji wa
madarasa makubwa yenye wanafunzi wengi huku wakitegemea kupata ufundishaji unaokidhi
viwango katika hali ya juu na dira ikiwa ni elimu kwa vitendo zaidi.
Yosepha
Hokororo, mwalimu mstaafu wa shule ya msingi Mkoani Lindi anasema kuwa madarasa
yenye wanafunzi wengi yanamnyima fursa mwalimu ya kujua tabia ya mwanafunzi
binafsi kutokana na ufinyu wa muda ukilinganisha na idadi yao.
“Wanafunzi
wakiwa wengi kupita kiasi katika darasa moja, wanafunzi wanashindwa kumsikiliza
mwalimu aliye mbele kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo usikivu mdogo hasa
kwa waliokaa viti vya nyuma ama waliokosa viti kabisa,” Mwl. Hokororo.
Akitolea
mfano katika shule mbalimbali za vijijini, Mwl. Hokororo anasema kuwa kuna
shule nyingi ambazo hazina walimu wakutosha hali ambayo huwafanya walimu
kutumia mbinu zisizo rasmi katika ufundishaji kwa wanafunzi wao.
“Uwiano
uliopo ni mwalimu mmoja kwa wanafunzi 125 kwa wakati mmoja ukiacha mikondo
mingine, inamuwia vigumu kusimamia utaratibu na
wakati mwingine zoezi la kuweka kumbukumbu za wanafunzi
linashindikana,”Anasema.
Akizungumzia
utendaji wa mwanafunzi mmojammoja, Mwl. Hokororo anabainisha wazi kuwa katika
darasa lenye idadi kubwa ya
wanafunzi hakuna upimaji mzuri wa maendeleo ya wanafunzi kutokana na ukweli kuwa mwalimu anaelemewa
na kazi nyingi za kufanya ikiwemo kuhifadhi kumbukumbu ya
kila mmoja.
ATHARI KISAIKOLOJIA
Kwa
mujibu wa Mwl. Hokororo, asilimia 20 ya wanafunzi walioko darasani ndio wenye
uwezo wa kuuliza maswali jambo linalosababishwa na ukosefu wa mwingiliano kati
ya walimu na wanafunzi kutokana na majukumu mengi.
“Hali hiyo inachangia kushusha ujuzi wa
mwalimu kwakuwa anakosa muda wa kutosha kusoma, kusikiliza, kubadilishana
mawazo pamoja na kufuatilia wanafunzi jambo ambalo humfanya mwalimu ashindwe
kufahamu upekee wa mwanafunzi wake,”Anasema.
Anaongeza
kuwa katika hali ya kawaida madarasa
kama haya huwa na mwingiliano mkubwa baina ya walimu na wanafunzi, hivyo ni
wanafunzi wachache tu ndio wanaopata
nafasi ya kuuliza ama kujibu maswali.
Aidha,
mstaafu huyo, anasema kuwa kutokana na hali halisi mwalimu anakosa nafasi ya
kukagua maendeleo ya mwanafunzi mmojammoja na kugundua yupi anahitaji msaada
wake wa karibu zaidi.
“Unakuta
tangu umeingia darasani na kufundisha hadi unatoka kati ya wanafunzi 78,
walioko darasani 20, tu wameuliza maswali na kujibu hali hiyo huchangia
wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kuelewa kudharaulika kutokana na walimu wao kuwa
na shughuli nyingi katika kufundisha jambo ambalo huwafanya wazidi kuwa dhaifu
zaidi,”Anabainisha.
“Madarasa
yenye msongamano yana madhara makubwa kwa wanafunzi kutokana na ukweli kuwa
unapunguza nafasi kwa shule kutoa elimu bora nchini,”.
Naye
Sebastian Namihambi, ambaye pia ni mwalimu mstaafu anasema ni vigumu kwa
mwalimu kufanya uchambuzi wa wanafunzi binafsi kwasababu jambo hilo linahitaji
muda zaidi.
Namihambi
anasema kuwa kutokana na wingi wa wanafunzi darasani, wachache kati yao ndio
hupata msaada wa mwalimu pindi wanapouhitaji lakini kadri wanavyoendelea
kushindwa hujijengea tabia ya kuchukia shule na kuamua kutoroka ama kukaa nje
ya madarasa.
“Kweli
walimu wanapata wakati mgumu sana hasa wanapotaka kusimamia na kufundisha
madarasa yenye wanafunzi wengi kwasababu kuwa wakati mwingine wanashindwa
kutumia mbinu mbalimbali za kufundisha,”
anasema Sebastian.
Sebastian
anafafanua zaidi kwamba hata pindi mwalimu anapoamua kutumia mbinu mbalimbali
za kufundisha inakuwa ngumu kwenye
madarasa yenye msongamano jambo ambalo hukwamisha elimu hiyo kuwafikia
wanafunzi wote kwa kiwango sawa.
Anasema
kuwa kutokana wingi katika madarasa walimu wanashindwa kutumia mbinu za ziada
kuleta ufanisi ikiwemo wanafunzi kupata nafasi ya kuuliza ama kujibu maswali
wakati wa kipindi.
“Licha
ya kusindwa kuelewa lakini pia ni hatari kwa afya kwasababu ufundishaji katika
madarasa yaliyofurika unaweza
kusababisha mzunguko wa hali hewa kutokuwa mzuri hivyo kuchangia magonjwa yanayoambukizwa
kwa njia ya hewa,” anasema Sebastian.
Anaongeza
kuwa idadi kubwa ya wanafunzi isiyo na uwiano na uwezo wa darasa inaathiri
uwezo wa wanafunzi kufuatilia kwa umakini ikiwemo kusikia na kusoma na
kusababisha matokeo duni.
“Ni
vigumu kwa mwanafunzi kutumia vifaa kwa vitendo kwa sababu hakuna uwiano uliopo
baina ya wanafunzi waliopo darasani na vifaa vya kufundishia vinayotumiwa na
mwalimu” Anafafanua.
“Uwiano
wa idadi ya wanafunzi ambao uliwekwa kipindi cha nyuma na iliyokuwa Wizara ya
Elimu na Utamaduni wa 1:40 ulidharauliwa, hivyo ni dhahiri kwamba hakutakuwa na
mafanikio mazuri wala usimamiaji mzuri wa nidhamu.
Kutokana
na hali hiyo Zainab Rashid, ambaye ni Mhadhiri msaidizi wa chuo cha Ustawi wa
Jamii anasema ipo haja kwa serikali kuweka vipaumbele katika ujenzi wa
miundombinu ya elimu pamoja na vitendea kazi.
Anasema
ili mtoto aweze kujifunza vizuri ni lazima kuwe na mahusiano mazuri katika
jamii jambo ambalo litaweza kumsaidia kwa kisai kikubwa.
Mwanasaikolojia
huyo anasema kisaikolojia mwanafunzi hujifunza vizuri kwa kushirikiana na
wenzake darasani wakiwa wachache jambo ambalo humpa fursa mwalimu kufuatilia
maendeleo yao.
“Ukifundisha
wanafunzi wachache huku ukiwagawa katika makundi wakashiriki vizuri inasaidia
kuwajengea uwezo wa kufanya vizuri kwani mwanafunzi asiposhirikishwa huathirika
kisaikolojia na kushindwa kuelewa anachofundishwa jambo ambalo humfanya akate tamaa,”
anasema.
Anasema
hali ya wanafunzi kushindwa kuelewa wanachojifunza kutokana na idadi kubwa darasani
humuatthiri walimu anayewafundisha.
“Wanafunzi
wasipoelewa mwalimu hukata tamaa ambapo wengine huacha kazi na kuamua kufanya
mambo mengine lakini wanafunzi wakiwa wachache humfanya anayewandisha
kuhamasika zaidi,”
Kutokana
na hali hiyo anasema serikali inapaswa kuandaa mazingira mazuri ya kusomeshea
wanafunzi ili waweze kujifunza na kuelewa vizuri.
NINI KIFANYIKE
Ili
kuboresha elimu kuelekea Tanzania tunayoitaka ipo haja kwa serikali kuongeza
nguvu katika kuwekeza kwenye seta ya elimu hususan kuboresha miundombinu na mazingira
rafiki kwa watoto ili kuwawezesha kujifunza kwa nadharia na kwa vitendo.
Hii
ina ukweli kwamba mazingira, miundombinu na idadi ndogo ya wanafunzi darasani humfanya
mwanafunzi ajifunze na kuelewa vizuri na kumfanya mwalimu ahamasike na
kuifurahia kazi yake,”
Mwanasaikolojia
huyo anasema wazazi hupeleka watoto wao kwenye shule za watu binafsi kutokana
na miundombinu rafiki iliyopo ambayo huwapa watoto fursa kujifunza kwa nadharia
na vitendo zaidi juambo ambalo huongeza kiwango cha ufaulu.
Pia
anasema serikali inalo jukumu la kuongeza walimu wa kutosha katika shule zake kwani
inaelezwa kuwa jumla ya walimu waliopo ni 88,999 ambapo kati yao 18,545
hufundisha masomo ya sayansi huku 70,454 wakifundisha masomo ya sanaa na
biashara.
Kuongeza
idadi ya walimu kutapunguza mzigo wa kufundisha masomo mengi hivyo watakuwa na
muda wa kutosha kufuatilia maendeleo na kufanya tathmini kwa wanafunzi wao.
Kadhalika
wazazi nao hawapaswi kukwepa jukumu la kujenga ushirikiano wa karibu na walimu
kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya watoto wao katika kujifunza kwao.
======================
COMMENTS