$type=slider$snippet=hide$cate=0

Jamii yakiwa kutoogopa vyombo vya habari kueleza kero

NA KOMBA KAKOA, Dar WANANCHI wametakiwa kuachana na kasumba ya kuogopa kutumia vyombo vya habari katika kueleza changamoto zinazowaka...


NA KOMBA KAKOA, Dar

WANANCHI wametakiwa kuachana na kasumba ya kuogopa kutumia vyombo vya habari katika kueleza changamoto zinazowakabili ili waweze kuisaidia serikali katika kuzipatia ufumbuzi.
Hali hiyo itaweza kuwawezesha kupatiwa maendeleo katika maeneo yanayowazunguka kutokana na kufikishwa mezani kwa viongozi wanaohusika.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Taasisi ya Waandishi wa Habari Vijini (TTAJA), Hassan Namkambe alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hizi juu ya ushiriki wa jamii katika kujipatia maendeleo kupitia vyombo vya habari.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo TTAJA imeamua kuanzisha mradi wa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa jamii isiyo na fursa ya kupaza sauti  vijijini unaojulikana kitaalamu kama Voice of Voiceless Communities kutumia vyombo vya habari kupaza sauti zao kuharakisha maendeleo yao.
“Mradi huu ni muhimu kulingana na wakati tulionao kwani uwazi ni muhimu ili kuongeza uwajibikaji wa mamlaka na jamii, kwamba ni  jambo mtambuka kwa ajili ya kuchochea kasi ya maendeleo hasa vijijini,” alisema Namkambe.
Alisema kuwa sehemu kubwa ya watu vijijini ni waoga kutumia vyombo vya habari  jambo ambalo kwalo kero zao zinashindwa kuifikia serikali huku wabunge wakishindwa kueleza kero zao bungeni  hivyo kuwa kizingiti cha  mipango na ndoto za wananchi wengi vijijini.
“Kutokana na hali hiyo TTAJA imekusudia kuanzisha elimu hiyo katika vijiji na wilaya zote za mkoa wa Kilimanjaro kisha mradi huo utahamia mikoa mingine na wilaya zote ili kufikisha elimu hiyo ambayo itakuwa chanzo cha jamii kujiletea maendeleo,” alisema.
Naye Katibu mkuu wa TTAJA, Abdala Sifi aliongeza kuwa ukosefu wa elimu ya matumizi ya vyombo vya habari kwa jamii zilizoko vijijini ni changamoto kubwa ambayo inawafanya washindwe kutatua mambo yanayowakabili.
“ Swala hili ni tatizo hasa ukiangalia matukio ya unyanyasaji wa kijinsia, uvunjifu wa haki za watoto yamesheheni vijijini kwasababu wananchi hawajatambua jinsi ya kujenga ukaribu na kuvitumia kutokana na uoga uliojengeka miongoni mwao,”alisema Sifi.
Kwa mujibu wa Sifi TTAJA itakuwa mkombozi kwa wananchi wanaoishi vijijini kutokana na elimu ya umuhimun wa vyombo vya habari katika kutatua changamoto zinazowakabili pamoja na kuwapatia maendeleo.
“Tumekusudia kuanza na wilaya Same mkoa wa Kilimanjaro ambako utafiti wa awali umeonyesha kuwa sehemu kubwa kuna mapungufu hayo. Elimu hii ya matumizi ya vyombo vya habari na matumizi sahihi ya vyombo hivyo hayalengi tu kuwajengea uwezo wananchi lakini tunachoangalia ni kuchochea uwajibikaji wa pande zote mbili, serikali kuu, serikali za mitaa na wananchi wenyewe kwa ujumla yaani Social Aaccountability Monitoring , (SAM),”alisema.
Hata hivyo Sifi alisema kuwa  taasisi yake inakabiliwa na ukata kutokana na kukosekana rasilimali fedha zinazowezesha kutekelezwa kwa mradi huo kwa ufanisi, na kuwaomba wadau mbalimbali kuwezesha taasisi yake kutekeleza mpango huo muhimu hasa vijijini.
 “Tunajua hapa nchini wapo wadau maendeleo kama vile Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Umoja wa wamiliki wa vyombo vya habari (MOAT), Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika hapa Tanzania (MISA-TAN),  Baraza la Habari Tanzania (MCT), TAMWA, serikali, taasisi na watu binafsi na wengine wa ndani na nje ya nchi wanaoweza kutuwezesha kusaidia kutekeleza mradi huu wenye faida kubwa ya kihabari kwa jamiiili (PIJ) ili kuendana na kasi ya sasa, ” alisema Sifi.

COMMENTS

Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Jamii yakiwa kutoogopa vyombo vya habari kueleza kero
Jamii yakiwa kutoogopa vyombo vya habari kueleza kero
https://1.bp.blogspot.com/-gmULldgN-7k/V77NTbc33kI/AAAAAAAAALQ/q3wpTjbbE348Gp4djCtvw0BmseLGIA0VwCEw/s400/HHH.JPG
https://1.bp.blogspot.com/-gmULldgN-7k/V77NTbc33kI/AAAAAAAAALQ/q3wpTjbbE348Gp4djCtvw0BmseLGIA0VwCEw/s72-c/HHH.JPG
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2016/08/jamii-yakiwa-kutoogopa-vyombo-vya_5.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2016/08/jamii-yakiwa-kutoogopa-vyombo-vya_5.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy