$type=slider$snippet=hide$cate=0

Sina mashaka na somo la Kinana ila hulka ya usaliti C

Na Felix Kalisa NIMESHANGAZWA na habari moja iliyoandikwa kwenye gazeti moja la kila siku ikiwataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi...



Na Felix Kalisa

NIMESHANGAZWA na habari moja iliyoandikwa kwenye gazeti moja la kila siku ikiwataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi, CCM kuhakikisha wanaibana serikali inayotokana na chama chao, ili itekeleze ilani na kuziba mianya ya ubadhirifu wa fedha za umma.
Kwa mujibu wa gazeti hilo ni kwamba; Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ndiye aliyetoa wito huo kwenye semina ya siku mbili ya wabunge wanaotokana na chama hicho, iliyofanyika hivi karibuni mjini Dodoma.
katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana
Hatua hiyo inadaiwa imelenga kuhakikisha wabunge wa vyama vya upinzani wanakosa kabisa hoja za kuikosoa bungeni na hatimaye kuidhohofisha kiutendaji Serikali ya Chama Cha Mapinduzi, inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli.
 Kwa mujibu wa habari hiyo; Kinana anadai wabunge wa vyama vya upinzani wamekuwa wakiibana serikali kwa kuikosoa na kufichua mianya yote ya ufisadi inayofanywa na viongozi mbalimbali wakiwa madarakani.
 Katika kikao hicho kilichoanza chini ya Kinana, kilidaiwa pamoja na mambo mengine kuwa na ajenda tatu ambazo ni Wajibu wa wabunge wa CCM kwa serikali, Tathmini ya Uchaguzi Mkuu uliopita na mchakato wa kura za maoni ndani ya chama.
Nasema nimeshangazwa na habari hiyo kwa sababu kuu moja; Ukiondoa utawala wa awamu ya kwanza, enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere na kabla ya ujio wa serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. Magufuli; kitendo cha wabunge wa CCM kuthubutu kukikosoa chama ama kufichua mianya ya wizi, rushwa na ufisadi unaofanywa na viongozi ni sawa na usaliti!
Hata vyombo vya habari vinavyomilikiwa na chama navyo vilijikuta vikinasa katika kasumba hiyo mbaya ya kusifu tu bila kukosoa kana kwamba Tanzania ni mbinguni na watawala ni miungu na malaika wasiofanya makossa.
 Ni katika mazingira kama hayo ndipo inasemekana wabunge wengi wa CCM wamekuwa wakilazimika kusifu tu na kupongeza kila jambo linalofanywa na chama chao, hata kama halina tija kwa umma na serikali huku pia wakisimama kidete kwa nguvu zote kupinga ukosoaji wowote ule dhidi ya serikali na chama chao hata kama ukosoaji huo una ukweli kwa asilimia mia moja!
Ndiyo maana sikushangaa kuwaona baadhi ya viongozi waandamizi, wabunge na makada ‘wazalendo’ wa chama hicho; waliowahi kuthubutu kukosoa ama kuibua kashfa dhidi ya wenzao ndani ya chama na serikali, wakiitwa wasaliti na waasi au wakiitwa kujadiliwa na kuhojiwa katika vikao vya juu vya chama; huku pia baadhi yao ama ‘wakiundiwa zengwe’ la kuangushwa kwenye uchaguzi kupitia kura za maoni ndani ya chama, ama wakati mwingine wakinyang’anywa uanachama na kufukuzwa.
Miongoni mwa waliowahi kukumbwa na dhahama kama hizo; ni pamoja na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Hayati Horace Kolimba baada ya kutofautiana na mwenendo mbovu wa chama chake na kuanika bayana kuwa chama hicho kimekosa dira na mwelekeo; Kolimba alifariki dunia mjini Dodoma Machi 13, 1997 muda mfupi baada ya mahojiano makali ndani ya vikao vya juu vya chama.
Mwingine ni mkongwe na muasisi wa mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 na mwanachama wa  CCM mwenye kadi namba 7, mzee Hassan Nassor Moyo aliyetimuliwa kwa kosa la kukosoa muundo wa muungano wa serikali mbili, ambao (kwa uhuru wake wa kutoa maoni kwa mujibu wa katiba ya nchi) anaona muundo huo hauna tija na umepitwa na wakati.
Mwingine pia aliyewahi kufukuzwa uanachama kwa sababu inayofanana na hiyo ya Mzee Moyo; ni aliyewahi kuwa Waziri Mwandamizi chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, (SUK) na mwakilishi wa jimbo la Kiembesamaki Mansour Yusuf Himid; achilia mbali baadhi ya wabunge machachari wanaodaiwa kutazamwa vibaya ndani ya chama kwa misimamo na uthubutu wao wa kuhoji, kukosoa na kukemea maovu ya viongozi ndani ya chama na serikali.
Hao ni pamoja na aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo la Ludewa (CCM) Hayati Deo Filikunjombe, Mbunge wa Simanjiro (CCM) Christopher Ole Sendeka, aliyewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kahama (CCM) James Lembeli, aliyewahi kuwa Mbunge wa viti maalumu (CCM) Bunda mjini kabla ya kuhamia Chadema na kuwa Mbunge wa kuchaguliwa wa jimbo hilo, Esther Bulaya; nawataja kwa uchache tu.
Nasema hivyo nikiwa na kumbukumbu ya mijadala ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusiana na kashfa mbalimbali zilizowahi kulikumba taifa letu na kulisababishia hasara kubwa ya mabilioni kwa matrilioni ya fedha ambazo zingetumika kulivusha taifa mbali sana kiuchumi na kijamii.
Kashfa hizo ni pamoja na ile ya wizi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), Kashfa ya mkataba wa kifisadi kati ya Shirika la Ugavi wa Umeme nchini, Tanesco na Kampuni ya kuzalisha umeme ya Richmond Development (LLC), sakata la wizi wa fedha za akaunti ya Tegeta Escrow, kashfa ya manunuzi ya Rada, Utoroshwaji wanyama, ujangili, madawa ya kulevya, akaunti tata za siri huko ughaibuni n.k.
Tulishuhudia migogoro yote hiyo ikifanyika ndani ya bunge letu kwa picha ya mapambano ya wabunge wa CCM waliokuwa wakiwawekea kifua watuhumiwa kwa kuwasafisha kadri walivyoweza, dhidi ya wabunge wachache wa upinzani waliotaka hatua kali zichukuliwe kwa mujibu wa sheria za nchi.
Hivyo basi badala ya wananchi kushuhudia wabunge wazalendo wa Tanzania bila kujali itikadi zao za vyama wakipambana dhidi ya wahalifu na uhalifu, wakajikuta wakishuhudia mapambano kati ya wabunge wa CCM dhidi ya wale wa upinzani hali iliyotafsiriwa kama vita ya CCM na Ukawa badala ya vita ya Bunge la Tanzania dhidi ya uhalifu na wahalifu.
Sasa sijui kama Bunge hili  la 11 (hasa kwa wabunge wa CCM), chini ya utawala wa awamu ya tano ya Rais Dk. Magufuli, litaweza kufanyia kazi maagizo hayo ya Katibu Mkuu wa CCM (taifa), Comrade Kinana ya kukosoa, kuibua maovu, kukemea na kuisimamia serikali kama wafanyavyo wabunge wa Ukawa.
Ni kwa njia hiyo pekee vyama vya upinzani vinaweza kudhohofishwa kisiasa bungeni na mbele za wananchi; kwa sababu kinachowafanya wao na hoja zao kuwa na nguvu ndani na nje ya bunge, ni kulinda na kutetea maslahi ya umma na taifa zaidi kuliko kuendekeza uchama.
Naweza kusema hiyo ndiyo tofauti kubwa kati ya wabunge wa CCM na wale wa vyama vya upinzani, kuhusiana na suala zima la wajibu wa bunge katika kuishauri na kuisimamia serikali kikamilifu, ili mapato yatokayo na kodi na utajiri mkubwa wa rasilimali za nchi, yaweze kuifaa nchi na wananchi wote bila kujali itikadi zao.
Lakini hoja ambayo Kinana anatakiwa kujiuliza ni kwanini anayoagiza wabunge wa CCM katika Bunge hili hayakutekelezwa katika bunge la 10, ili-hali yeye na timu ya viongozi wenzake walifanya ziara kwenye mikoa mbalimbali na agenda kuu ya mikutano ya ziara hizo ilitawaliwa na karipio dhidi ya viongozi wa umma na hata ikafikia kuwaita baadhi ya mawaziri waliotokana na CCM kuwa ni mizigo? Tungoje tuone wabunge wa CCM wenye ujasiri wa kutekeleza kile anachotaka Kinana.
Ni muhimu pia kutambua kuwa changamoto hii inayotolewa na Kinana kwa wabunge wake ni juhudi ya wapinzani kuibua uovu wa viongozi, lazima Kinana atambue kuwa wapinzani nao watakuja na mipango na mikakati yao mipya.
0655 872873,  0784 872873.
==============
Imetumika TAIFA LETU

COMMENTS

Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Sina mashaka na somo la Kinana ila hulka ya usaliti C
Sina mashaka na somo la Kinana ila hulka ya usaliti C
https://1.bp.blogspot.com/-Ugfh82oB28Q/V9KkE1z3_7I/AAAAAAAAAMA/-swsu1ZAL8o9N-N5M2fKg_5ZVszSkYZ_wCLcB/s400/Kinana.jpg
https://1.bp.blogspot.com/-Ugfh82oB28Q/V9KkE1z3_7I/AAAAAAAAAMA/-swsu1ZAL8o9N-N5M2fKg_5ZVszSkYZ_wCLcB/s72-c/Kinana.jpg
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2016/01/sina-mashaka-na-somo-la-kinana-ila.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2016/01/sina-mashaka-na-somo-la-kinana-ila.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy