$type=slider$snippet=hide$cate=0

Lowassa amlizamtoto wa Sokoine

     CCM yamtaka asikubali kurubuniwa   Yamuahidi Ukuu wa Wilaya akishindwa   MGOMBEA ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (...



     CCM yamtaka asikubali kurubuniwa

 Yamuahidi Ukuu wa Wilaya akishindwa 





MGOMBEA ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) jimbo la Monduli, mkoani Arusha, Namelock Sokoine, amejikuta akiangua kilio mbele ya mgombea urais
kupitia Chadema Edward Lowassa baada ya mwanasiasa huyo anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa  kumtamkia kuwa hamuungi mkono tena.
Namelock ambaye ni mtoto wa Waziri Mkuu wa zamani Edward  Sokoine, yupo kwenye harakati za kutaka kumrithi Lowassa aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa muda mrefu.
Kutokana na Lowassa kuwa mgombea imara  na mzito katika Jimbo la Monduli, Namelock alitegemea angepata sapoti kubwa toka kwake hali ambayo imekuwa kinyume.
Tukio la kuangua kilio lilitokea mjini, Babati katika kikao cha ndani ambacho kiliwakutanisha wagombea wa Chadema katika jimbo hilo pamoja na mgombea wa CCM,Namelock, akiwa  na familia yake.
Kikao hicho kiliitishwa na  Lowassa baada ya kuwepo na taarifa za kizushi na za kipropaganda zilizodai kuwa Namelock bado anaungwa mkono na Lowassa Ikumbukwe kuwa wakati Lowassa akiwa katika harakati za kutaka urais kupitia CCM, Namelock alikuwa ‘mtu wake’.
Katika tukio hilo Lowassa alianza kuzisikiliza pande mbili ambazo zilizokuwa zikisigana kuhusu nani hasa anastahili kuungwa mkono kuwa mbunge wa jimbo la Monduli.
Katika Jimbo hilo Chadema kimemsimamisha, Julias Kalanga huku CCM wakimsimamisha Namelock.
Awali Namelock alilalamika hatua ya yeye kutukanwa na kuzalilishwa na mgombea wa viti maalum wa jimbo hilo (Chadema) Cesilia Ndosi.
Alimweleza Lowassa   kuwa Cesy amekua akimwambia kuwa hajasoma na wala hajawahi kuwa na cheo chochote shuleni hivyo ni dhaifu hafai kuwa mbunge katika jimbo la Monduli
Kwa upande wake Cesy alimweleza Lowassa kuwa ni kweli maneno hayo amekuwa akiyasema jukwaani kwa kuwaeleza wananchi kuwa mgombea huyo  hana elimu, kwani  alisoma naye sekondari na hawezi kuwaongoza wananchi wa Monduli.
Hata hivyo alimtaka Lowassa awaeleze kinaga ubaga ni nani anafaa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Baada ya ombi hilo ndipo Lowassa alipotamka wazi kwa kumweleza Namelock kuwa alimpenda awe mrithi wake katika jimbo hilo wakati akiwa CCM lakini wakati huu amempenda zaidi Kalanga wa Chadema, baada ya kujiengua kwenye Chama hicho kinachotawala.
Lowassa alimshauri Namelock aachane na ubunge katika jimbo hilo na amfuate Chadema na hatimaye Ukawa hatua ambayo ilimfanya Namelock aangue kilio.
Binti huyo aliendelea kuangua kilio zaidi pale Lowassa alipomshika mkono Kalanga na kuwaambia watu “Jamani huyu ndiye mwanangu mpendwa ninayependezwa naye, mpeni kura.”
Hata hivyo habari toka CCM zinasema kuwa CCM iliunda timu ya watu wazito kwenda Monduli kumshawishi Namelock asikubali kuhama CCM kwa madai kuwa hata akishindwa atapewa hata Ukuu wa Wilaya.
Imeelezwa kwamba timu hiyo ilipitia pia kwa wazazi wa Namelock kwa lengo la kumtisha binti huyo.
CHANZO: TAIFA LETU

COMMENTS

Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Lowassa amlizamtoto wa Sokoine
Lowassa amlizamtoto wa Sokoine
http://3.bp.blogspot.com/-6NZUOssNsko/VhUhApdzZaI/AAAAAAAAAIg/YM2psIJb6II/s400/Lowassa.jpg
http://3.bp.blogspot.com/-6NZUOssNsko/VhUhApdzZaI/AAAAAAAAAIg/YM2psIJb6II/s72-c/Lowassa.jpg
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2015/10/lowassa-amlizamtoto-wa-sokoine.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2015/10/lowassa-amlizamtoto-wa-sokoine.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy