Waziri wa fedha anayemaliza muda wake, Saada Mkuya TAKWIMU zinaonyesha kuwa hadi kufikia mwezi ...
Waziri wa fedha anayemaliza muda wake, Saada Mkuya |
Wakati
taifa likiandamwa na madeni, takwimu pia zinaonyesha kuwa kasi ya kukopa na
misamaha ya kodi imekuwa kubwa kuliko ile ya kulipa deni la taifa. Kwa mfano
kuanzia mwezi Julai 2014 hadi April mwaka huu, misamaha ya kodi ilifikia Sh.
trilioni 1.3 sawa na asilimia 1.4 ya pato la taifa.
Pamoja
na hayo yote, tunaambiwa kuwa katika mwaka huu wa fedha jumla ya Sh. trilioni
16 zimetengwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida huku shughuli za maendeleo
zikitengewa Sh.trilioni sita tu.
Aidha
Serikali imekuwa ikilalamika kuwa baadhi ya wafadhili hawatekelezi ahadi zao za
kuichangia bajeti, na hivyo kuilazimu Serikali kukopa fedha kutoka benki ili
kuendesha mipango ya maendeleo.
Kwa
mfano, Ilielezwa na wabunge wakati wa uwasilishaji wa bajeti ya mwaka 2012/13
kuwa katika bajeti iliyotangulia kabla ya mwaka huo wa fedha, takribani
asilimia 40 ya fedha zilizotarajiwa kutolewa na wafadhili hazikupatikana.
Hivyo
maana yake ni kwamba, miradi iliyopangiwa fedha za maendeleo kutoka kwa
wafadhili haikutekelezwa kwa asilimia mia moja.
Hata
hivyo, Serikali hiyo hiyo, ambayo asilimia 75 ya bajeti zake huelekezwa kwenye
matumizi, imekuwa kinara wa kuendekeza misamaha ya kodi kwa makampuni makubwa
na kulimbikiza deni la taifa. Kwa upande mwingine, wafadhili wanaoridhia
kuichangia bajeti ya serikali, wamekuwa na masharti mbalimbali.
Mara
kadhaa serikali ya Tanzania imekuwa ikipewa masharti na Shirika la Fedha
Duniani (IMF), la kuhakikisha kuwa inaweka umakini mkubwa katika kukusanya kodi
na kutii misingi ya Utawala Bora.
Tunapoelekea
Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, wananchi wanao wajibu wa kuwahoji wanasiasa kujua
fedha zinazo kopwa zinaztumikaje? misingi ya kukithiri misamaha ya kodi kwa
makampuni ya uwekezaji na ulegevu wa mifumo ya ukusanyaji kodi.
Kwa
kiwango cha misamaha ya kodi kinavyopaa na deni la taifa kuzidi, Tanzania inahitaji
Serikali ya awamu ya tano kuwa makini na ukusanyaji kodi, mipango madhubuti ya
kutolimbikiza deni la taifa.
Kuna
ulazima kwa Watanzania kujua mchanganuo wa matumizi wa fedha zinazokopwa iwapo
ni kwa shughuli za maendeleo ama matumizi ya posho, ziara, semina, mishahara na
mambo mengine yanayohitaji serikali kuwa wazi (Open Government).
Mgombea urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo, Anna Mghwira |
Misamaha
ya kodi iliyotolewa kwa mashirika na makampuni binafsi, iliikosesha serikali
mapato y a Sh. trilioni 1.03 kwa mwaka wa fedha 2011/12.
Katika
Taarifa ya Utafiti ya mwaka 2010, iliyotolewa na taasisi iliyoitwa `The One
Billion Dollar Question’, inaonyesha kuwa kabla ya bajeti ya mwaka
2011/12,Tanzania ilikuwa imepoteza takribani Sh. trilioni 1.7 kutokana na
misamaha ya kodi,ukwepaji wa kodi, udanganyifu kwenye biasha ya kimataifa na utoroshwaji
wa mitaji nje.
Udhaifu
katika kukusanya mapato uliifanya serikali kukosa fedha za kutosha kutekeleza
bajeti ya sh trilioni 13 iliyoidhinishwa na Bunge kwa mwaka wa fedha 2011/12.
Hadi
kufikia 2011/12, Deni la taifa lilikuwa sh trilioni 22 kutoka sh trilioni 13 ya
mwaka 2010/11, kutokana na serikali kukopa kwenye Benki za Biashara na Shirika
la Fedha Duniani.
Suala
la kutokukusanya kodi ipasavyo, linamuongezea mzigo mwananchi wa kawaida
kupitia bidhaa za lazima anazotumia, kupanda bei kila leo na makato lukuki kwa
wafanyakazi ukilinganisha na kiwango cha mishahara yao.
Mgombea urais kwa tiketi ya Ukawa, Edward Lowassa |
Katika
bajeti ya mwaka 2012/13 iliyoelekezewa Sh. trilioni 15.Trilini 10 zilitengwa
kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo zilitengewa Sh. trilioni tano tu.
Bajeti ya mwaka 2012/13 pia ilionyesha kuwa, serikari ilitarajiwa kukusanya Sh.
trilioni 8.7 kama makusanyo ya kodi ya ndani ambapo ilipanga kutumia Sh.
trilioni 10.6 kwa matumizi ya kawaida. Kwa mchanuo huu, Serikali ilikuwa lazima
itumie fedha ya mkopo kwa matumizi ya kawaida. Katika bajeti hiyo hiyo, Serikali
iliainisha kuwa ilitakiwa kukopa Sh. trilioni 5.
Ripoti
iliyotolewa mwezi Oktoba mwaka jana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG), ilisema kuwa misamaha mikubwa ya kodi ilisababisha pengo la
asilimia 10 ya bajeti ya mwaka wa fedha 2012/13. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, iliyowasilishwa
Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali Kuu (PAC), misamaha ya kodi ilikuwa ni
zaidi ya trilioni 1.5 sawa na asilimia 10 ya bajeti ya mwaka huo iliyoelekezewa
Sh. trilioni 15.191.
Fedha
zinazopotea kupitia misamaha ya kodi ni kubwa kuliko fedha zinazotolewa na
wahisani.Kwa mfano, katika bajeti ya mwaka 2012/13, fedha zilizotolewa na
wahisani zilikuwa sh trilioni 1.3.
Hii
inamaanisha kwamba, fedha hizo Serikali isingeweza kuzikopa iwapo tu
isingeendekeza misamaha ya kodi kwa sababu ingekuwa nayo mfukoni.
Kwa
kukokotoa, Sh trilioni 1.5 iliyopotea ingeweza kusaidia upatikanaji wa huduma
nyigine za jamii.Kwa mfano kama dawati moja la kiwango cha juu, linakadiliwa
kuwa na thamani y ash 140,000/=,fedha hii ingeweza kutumika kununulia madawati
zaidi ya milioni 10 na hivyo kumaliza kabisa tatizo hilo kwa shule nyingi
nchini.
Ni
aibu kubwa kwa nchi yenye rasilimali nyingi kuzungumzia uhaba wa madawati kwa
kipindi cha zaidi ya miaka 50 tangu uhuru.
Aidha,
fedha hizo zingeweza kutumika kugharimikia uchimbaji wa visima virefu vya maji,
kuimarisha miundombinu ya barabara, kujenga zahanati zakutosha na pia kumaliza
tatizo la mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu nchini.
Kwa
upande mwingine, kama Sh. trilioni 1.5 zimgekusanywa kupitia mfumo wa kodi, zingeweza
kutumika kukamilisha ujenzi wa maabara zenye thamani ya wastani wa Sh. milioni
mia moja kwa kila moja.
Serikali
isingekuwa inaumiza kichwa tena kwa tatizo hili linazozikabili shule nyingi na
wananchi wasingesumbuliwa kwa michango ya miradi hiyo, kwani fedha hizo
zingetosha kukamilisha ujenzi wa maabara 15,000.
Mwaka
2012 takwimu zinaonyesha kuwa deni la taifa liliongezeka kwa asilimia 15.2
ndani ya mwaka mmoja wa fedha kutoka Sh. bilioni 18.2 mwaka 2011 na kuwa
bilioni 21 mwaka 2012.
Kati
ya fedha hizo deni la fedha za nje lilikuwa asilimia 75.95. Sababu iliyoelezwa
na serikali kuwa lilitokana na mikopo mipya kwa ajili ya kugharimikia barabara,
umeme na malimbikizo ya riba ya mikopo ya nyuma.
Serikali
ilitenga sh trilioni 19.7 kwa ajili ya bajeti ya mwaka wa fedha 2014/15. Sehemu
kubwa ya bajeti hiyo ilitengwa kwa ajili ya kugharimikia uchaguzi wa serikali
za mitaa mwaka 2014, maandaalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu na kukamilisha
rasimu ya katiba mpya.
Bajeti
hiyo ilikuwa na ongezeko la sh trilioni 1 toka bajeti ya mwaka 2013/14.
Akiwasilisha
bajeti ya serikali bungeni ya mwaka 2015/16,Waziri wa fedha,Saada Mkuya Salum
alisema,serikali imeweka mapendekezo kwenye muswada wa fedha wa mwaka
2015/16,wa namna ya kutambua wawekezaji mahususi wa kimkakati ambao watapewa
misamaha ya kodi itakayo pendekezwa na waziri wa fedha ili kupata idhini ya
bunge.
Sifa
za mwekezaji huyo ni kuwa na mtaji usiopungua dola milioni 300 za Marekani na
mtaji wa kifedha unapaswa upitie kwenye taasisi za fedha zilizopo nchini.
Pamoja
na uwekezaji wake huo utoe ajira kwa watanzania wasiopungua 1,500. Katika
bajeti hiyo, serika liimekadilia kutumia sh trilioni 22.495, ambazo ni Sh.
trilioni 16.576 kwa ajili ya matumizi ya kawaida, wakati shughuri za maendeleo
zimetengewa Sh. trilioni 5.919 ambazo ni idogo kuliko fedha zitakazokopwa
kufidia nakisi katika bajeti.
Waziri
wa fedha, Saada Mkuya, wakati akiwasilisha bajeti hiyo, alisema serikali
inatarajia kukopa kutoka katika vyanzo vya ndani nan je kiasi cha Sh. trilioni
6.175 ili kuziba nakisi inayotokana na kiwango kikubwa cha matumizi
ikilinganishwa na mapato.
Wakati
serikali ikijipanga kupata kiasi hicho cha fedha, waziri Mkuya aliliambia Bunge
kuwa hadi machi mwaka huu, deni la taifa lilikuwa limefikia dola za Marekani
bilioni 19.5 sawa na Sh. trilioni 35. Fedha ambazo zinatosheleza kugharimikia
bajeti nzima ya mwaka 2015/16 na kubaki, ikilinganishwa na Sh. trilioni 30.6
machi 2014 ya deni la taifa.
Licha
ya waziri Mkuya kusema serikali imeendelea kupunguza utegemezi wa bajeti kutoka
asilimia 24 mwaka 2004/05, asilimia 17 mwaka 2010/11 na kufikia asilimia 6.4
mwaka 2015/16.
Ukweli
unabaki kuwa haauna faida yoyote ikiwa zimetengwa fedha nyingi za bajeti kwa
ajili ya matumizi na zile za shughuli za maendeleo kusuburi fedha za wahisani.
IMETUMIKA:TAIFA LETU
IMETUMIKA:TAIFA LETU
COMMENTS