SHERIA ya makosa ya mitandao ilianza kutumika Septemba Mosi, mwaka huu baada ya kupitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tan...
SHERIA
ya makosa ya mitandao ilianza kutumika Septemba Mosi, mwaka huu baada ya
kupitishwa na Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya
Kikwete.
Baada
ya hatua ya rais kuisaini sheria hiyo maana yake sasa usimamizi wa utekelezaji
wa sheria hiyo utasimamiwa na vyombo vya dola yaani Jeshi la Polisi na
Mahakama.
Sheria
hiyo kabla ya kusainiwa na kuanza kutumika ililalamikiwa na makundi mbalimbali
ya jamii na kuzua mjadala mkali miongoni mwa wananchi, ambao wamekuwa wakitumia
mitandao ya kijamii kwa shughuli zao mbalimbali za kila siku.
Kubwa
zaidi ni kuwa makundi hayo yalilalamikia hatua ya serikali ya kufanya
maandalizi bila ushirikishaji wa jamii kupitia wadau ili watoa maoni yao
kuhusiana na jinsi gani sheria hiyo iwe; kwa maana ni mambo gani yaingizwe
kadri wangeona inawafaa.
Kutokuwashirikisha
wadau kulitafsiriwa kwamba serikali haikuwa na nia njema, bali nia ovu ambayo
lengo lake ni kudhibiti uhuru wa jamii kupashana habari, jambo ambalo ni haki
ya msingi kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Tunapozungumzia
haki ya kupeana taarifa maana yake ni kwamba jamii iwe huru kutumia vyombo vya
mawasiliano zikiwamo redio, televisheni, magazeti, majarida na mitandao ya
kijamii ilimradi sheria za nchi zifuatwe.
Ili
kuhakikisha kuwa vyombo hivyo vinatumiwi vibaya kukiuka sheria na kuingilia
uhuru wa watu binafsi, ndiyo maana serikali ilitunga sheria kuanzia ya magazeti
ya mwaka 1976 na ya utangazaji ya mwaka 1993.
Hizi
sheria hususan ya magazeti ambayo imekuwa ikitekelezwa sambamba na Sheria ya
Usalama wa Taifa namba 20 ya mwaka 1970 kwa miaka mingi, imekuwa ikilalamikiwa
sana kutokana na kumpa Waziri mamlaka makubwa ikiwamo kulifungia gazeti lolote
kwa muda usiojulikana bila hata kusikiliza utetezi.
Sheria
hiyo iliorodheshwa na Tume ya Nyalali ya mwaka 1991 kuwa ni miongoni mwa sheria
mbaya ambazo zilipaswa kufutwa, lakini hadi leo serikali imekaa kimya na
inaendelea kutumiwa kufungia magazeti.
Kuna
orodha ndefu ya magazeti ambayo waziri aliyafungia kwamuda usiojulikana na
mengine kupewa amri ya kusimamisha uchapishaji kwa miezi kadhaa kwa maelezo ya
kukiuka maadili, lakini bila kupewa haki ya kuwasilisha utetezi.
Tume
ya Jaji Nyalali ilisema sheria hiyo na nyingine zipatazo 40 zimepitwa na
wakati, hivyo zifutwe kwa sababu hazifai kutumika katika nchi ya kidemokrasia
inayofuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
Sheria
ya Makosa ya Mitandao ina maeneo kadhaa ambayo lengo lake ni kudhibiti matumizi
mabaya. Miongoni mwa maeneo yanayoguswa nasheria hiyo ni pamoja na kusambaza
ujumbe wa uchochezi kupitia mitandao ya kijamii.
Serikali
iliandaa sheria hiyo kwa kueleza kuwa ina lengo la kudhibiti matumizi mabaya ya
mitandao ya kijamii ikiwamo ya Watsapp, Facebook, Youtube, Instagram na
mingine.
Pamoja
na maelezo hayo ya serikali kwamba lengo la kutungwa kwa sheria hiyo ni mazuri,
lakini makundi kadhaa ya jamii hayakuridhishwa na maelezo hayo na kuendelea
kuhoji kuhusiana na kuandaliwa kwa sheria hiyo pamoja na kusainiwa na rais kuwa
sheria kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Kuna
watu wanaamini kuwa lengo la sheria hiyo ni kudhibiti uhuru wa maoni ya
wananchi na hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi huo wa rais,
wabunge na madiwani. Katika mazingira hayo, hisia za watu hao hazipaswi
kupuuzwa kutokana na uzoefu ulioko nchini; kwamba wakati wa uchaguzi maamuzi
mengi ya ghafla na ya kushangaza hufanyika na kuzua maswali katika jamii.
Watu
hao wanaamini hivyo kutokana na moja ya vifungu vya sheria hiyo kupiga marufuku
ujumbe wa uchochezi ama ushawishi wa kisiasa unaoweza kuleta athari kwa jamii
kupitia mitandao.
Pia,
sheria hiyo inabana kuhusu masuala ya kusambaza au kutunga ujumbe unaoleta
uchochezi wa kidini unaoweza kusababisha kuvuruga amani na maelewano ndani ya
jamii kupitia mitandao.
Sheria
hiyo inaeleza wazi kwamba wavunjaji wa sheria husika wanaweza kukabiliwa na
vifungo vya gerezani au faini ya fedha isiyopungua Shilingi milioni tano
kulingana na kosa lililofanyika.
Kutokana
na ukweli kuwa sheria yenyewe ilishapitishwa na wabunge, ni vizuri sasa
Watanzania wakazingatia utekelezaji wake ili kujiepusha adhabu zilizoainishwa.
Mathalan,matumizi
ya mitandao yamekuwa ya kiwango cha juu katika kipindi hiki cha kuelekea
Uchaguzi Mkuu.
Mitandao
hiyo imekuwa ikitumika kwa njia mbalimbali zikiwamo kampeni miongoni mwa
wagombea, lakini pia kuna baadhi ya watu wamekuwa wakiitumia kuwashambulia,
kuwakashifu, kuwatukana, kuwatisha wenzao na mambo mengine ya ovyo.
Kadhalika,
mitandao hiyo imekuwa ikitumika vibaya na kuwazushia mambo, kuwatukana na
kuwadhalilisha watu mbalimbali wakiwamo viongozi wa kitaifa.
Pamoja
na ukali wa sheria yenyewe, ni vizuri wananchi wakaisoma na kuielewa sheria
hiyo ili kujiepusha na matatizo yanayoweza kuwakuta huko mbele ya safari.
Sheria
hiyo ni kali na inadhibiti baadhi ya maeneo na hasa yale ya utoaji wa maoni,
lakini sisi kama taifa inabidi tukubali kuwa taifa letu katika kipindi hiki
linahitaji miongozo ya kudumisha amani na utulivu.
Kimsingi,
lengo la kuanzishwa kwa mitandao ya kijamii ni zuri kwa lengo la kupashana
habari kwa urahisi, lakini kwa bahati mbaya sana, baadhi ya watu wamebadili
matumizi yake.
Siku
hizi mitandao ya jamii imegeuzwa kuwa sehemu ya kuzushia watu mabaya. Si ajabu
kusoma kwenye mitandao kuwafulani kafa wakati ni uongo. Nakumbuka kuna siku
mtandao mmoja ulidai kuwa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru,
amefariki dunia wakati haikuwa kweli.
Mara
kadhaa katika mitandao zimekuwa zinaandikwa habari za uzushi kuhusu kutokea kwa
ajali za barabarani wakati siyo kweli.
Hivi
karibuni, mtandao mmoja uliandika kuwa Makamu waRais, Dk. Mohamed Gharib Bilal,
alikuwa na mkutano na vyombo vya habari katika moja ya hoteli za kitalii,
jijini Dar es Salaam kuelezea hatma yake ya kisiasa wakati haikuwa kweli.
Katika
mazingira kama haya, nchi haiwezi kwenda wala kutawalika, ni lazima mitandao
itumike pamoja na mambo mengine, kuheshimu uhuru wa watu, haki, faragha na
kuhakikisha kuna amani na utulivu wa nchi.
Kwa
kuwa tayari muswada uliokuwa unalalamikiwa na wadau umeshakuwa sheria, ni
muhimu sana kwa wananchi kuisoma vizuri sheria hiyo na kuielewa kwa kuwa
atakayefanya makosa atashughulikiwa bila kusamehewa kwa kuwa kutojua sheria
siyo utetezi (ignorance of law has no defence).
Sheria
ikishasainiwa kinachobakia ni utekelezaji wake, kila mmoja ahakikishe
anajiepusha na kitendo chochote ambacho kitakiuka sheria hiyo kwa kuwa matokeo
yake itakuwa ni kufungwa jela au kutozwa faini.
Kwa
kuwa serikali ilishasema kuwa kama yataonekana mapungufu wakati wa utekelezaji
wake itakuwa tayari kuipitia, ni vizuri itekeleze ahadi hiyo kwa kuwa
upitishaji wake uliacha maswali mengi kuliko majibu kutoka kwa wananchi.
Waziri
wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, aliyetoa ahadi
hiyo hanabudi kuhakikisha utaratibu wa kupata maoni ya wadau unaanzishwa ili kuangalia uwezekano wa kuiboresha sheria hiyo
itekelezwe bila kuwapo malalamiko na manung’uniko kutoka kwa jamii.
IMETUMIKA TAIFA LETU
COMMENTS