Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba NISHATI ya umeme limekuwa ni tatizo ambalo limewaathiri Watanzania kwa miaka mingi bila k...
Mkurugenzi wa Tanesco, Felchesmi Mramba |
NISHATI
ya umeme limekuwa ni tatizo ambalo limewaathiri Watanzania kwa miaka mingi bila
kupatiwa ufumbuzi wa kudumu.
Shida
ya umeme ilianza kuitikisa nchi tangu uongozi wa awamu ya pili ya Ali Hassan
Mwinyi na kurithiwa na awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa ambaye naye alimrithisha
Rai wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete.
Rais
Kikwete naye analiacha tatizo hilo kwa rais wa awamu ya tano ambaye atajulikana
mwishoni mwa Oktoba mwaka huu baada ya uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika
Oktoba 25.
Kutokana
na tatizo hilo, serikali zote zimejaribu kuchukua hatua ikiwamo kuingia katika
mikataba na kampuni mbalimbali za kufua umeme wa dharura.
Kwa
mfano, serikali ya awamu ya pili iliingia katika mkataba na Kampuni ya
International Power Tanzania Limited (IPTL) mapema miaka ya tisini kwa lengo la
kunusuru hali hiyo.
Hata
hivyo, pamoja na mkataba huo kuonekana kuwa wa kinyonyaji na kuibua malalamiko
kuwa serikali haikuwa makini wakati wa kusaini mkataba huo, bado matatizo ya
nishati hiyo yaliendelea.
Moja
ya kuongezeka wka mahitaji hayo ni kutokana na mvua kutokuwa za uhakika na
kusababisha mabwawa yaliyojengwa kwa ajili ya kuzalisha umeme kukauka mara kwa
mara.
Adha
ya kukauka kwa mabwawa ya Mtera, Kidatu, Nyumba ya Mungu na mengine imekuwa
ikishuhudiwa mara kwa mara pale mvua zinapokosekana au kunyesha kwa kiwango
kidogo.
Kwa
mfano, mwaka 2006 nchi ilikumbwa na janga kubwa la ukame lililosababisha
kukauka kwa mabawawa na kutishia nchi kuingia gizani. Serikali iliamua
kuingilia kati haraka kwa kuingia katika mkataba mwingine na kampuni ya kuzalisha
umeme ya Richmond ya Marekani.
Ingawa
kampuni hiyo ilibainika kuwa haikuwa na uwezo wa kuzalisha umeme na kwamba
ilipewa zabuni kwa upendeleo, lakini ilipewa zabuni ya kuzalishamegawati 100
kwa gharama ya takribani Shilingi bilioni 180.
Sina
lengo la kujadili masuala ya IPTL wala Richmond ambayo yamegeuzwa siasa, lakini
ninachotaka kueleza hapa ni jinsi gani Watanzania wanaendelea kuumizwa na tatizo
la umeme bila sababu za msingi.
Ingawa
baada ya serikali kujikita katika uchumi wa gesi; kwa maana ya kuanza kuitumia
kama chanzo cha nishati, Watanzania wameanza kujenga matumaini ya kuondokana na
adha hiyo, lakini bado serikali inawasababishia adha bila sababu za msingi.
Shirika
la Umeme nchini (Tanesco), Jumapili iliyopita, lilitangazia umma kwamba nchi
nzima itakuwa gizani kwa takriban wiki nzima kuanzia Jumatatu.
Shirika
hilo lilieleza kuwa hali hiyo inatokana na kuzimwa kwa mitambo ya gesi inayozalisha
umeme kutoka Songosongo mkoani Lindi.
Kwa
mujibu wa Tanesco, lilichukua hatua hiyo kutokana na kazi ya kuunganisha bomba
la gesi kutoka Mtwara na mtambo wa umeme wa Kinyerezi II.
Hatua
hiyo ilianza kuwaathiri wananchi kuanzia Jumatatu baada ya baadhi ya mitambo ya
kuzalisha nishati hiyo kuzimwa kwa ajili ya kutekeleza kazi hiyo.
Uamuzi
wa Tanesco pamoja na kwamba ni mchungu kwa watumiaji wote wa umeme, lakini
dhamira yake njema na lengo lake ni kuboresha utoaji huduma ya umeme
nchini ambayo kwa miaka nenda rudi, imekuwa haikidhi matarajio ya wateja wake
na Watanzania kwa ujumla.
Hata
hivyo, Tanesco hawakutumia busara sana katika kutekeleza kazi hiyo kwani
hawakushirikisha wateja wao na umma kwa ujumla.
Dunia
ya leo inaendeshwa kwa uwazi na ushirikishaji, hivyo Tanesco ilipaswa
kuwashirikisha wateja wake na umma kwa ujumla kwa kuwapa taarifa mapema kwa
kuwa kazi ya kuunganisha bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara na mitambo yake,
ilikuwa imepangwa kwa muda mrefu.
Kazi
hiyo haikuwa ya dharura, lakini wateja na umma ulijulishwa kwa dharura yaani
siku mpja kabla ya kazi hiyo kuanza kutekelezwa.
Kwa
nini taarifa isingetolewa mwezi mmoja kabla ili watumiaji wa umeme wajiandae
kuchukua hatua za kukabiliana na athari ya kukosa umeme kwa wiki nzima?
Watumiaji
wa umeme wanatofautiana katika matumizi ya nishati hiyo kwa kuwa kuna wamiliki
wa viwanda vikubwa, viwanda vidogo, taasisi, wafanyabiashara na watumiaji wa
kawaida.
Wote
hao kila mmoja alitakiwa kupewa taarifa mapema akajiandaa kwa kupanga bajeti
yake. Wapo ambao wangehitaji kununua jenereta, mafuta ya kuendesha jenereta,
kununua taa, mishumaa na vifaa vingine ili kuhakikisha kwamba shughuli zao
hazikwazwi kwa kukosa umeme kwa wiki nzima.
Katika
muktadha huo, shirika hilo lingetakiwa kutoa taarifa ili wahusika wajipange kwa
ajili ya kukabiliana na makali hayo.
Wamiliki
wa viwanda wana mahitaji makubwa ya umeme na nishati hiyo ndiyo inayowezesha
viwanda vyao kuzalisha, hivyo walihitaji taarifa ya muda mrefu ili wafanyie matengenezo
jenereta zao.
Mbali
na viwanda ambavyo kwa asilimia kubwa hutegemea umeme wa shirika hilo, lakini
pia wajasiriamali mbalimbali hutegemea nishati ya umeme kuendeshea shughuli zao
za kiuchumi kama vile saluni za kike na kiume, inateneti, gereji za magari,
wauzaji wa vinywaji baridi na vikali, wauza samaki, juisi, na nyama, mama
ntilie, wachomeleaji vyuma; kutaja baadhi.
Aidha,
hatua hii ya Tanesco kwa kiasi kikubwa pia itaathiri uzalishaji wa viwandani
kwani vitalazimika kuingia gharama za kutumia majenereta yanayotumia mafuta.
Matumizi
ya jenereta, ni wazi kwamba yatachangia kwa kiasi kikubwa kupandisha bei ya
bidhaa zinazozalishwa viwandani na hivyo kuongeza ugumu wa maisha kwa wananchi.
Viwanda
vingi vinaendeshwa kwa bajeti na hatua hii ya Tanesco kuzima ghafla mitambo
yake, italeta athari kubwa.
Mbali
na shughuli hizo za kiuchumi, lakini pia kuna masuala ya kijamii kama shughuli
za hospitali kwani kwa hatua hii ya Tanesco, ni dhahiri wagonjwa wengi
wanaohitaji huduma za matibabu wataathirika.
Kwa
kuwa Watanzania bado wanakumbuka adha ya umeme ya muda mrefu, ni vizuri
wangepunguziwa mzigo wa mgawo wa umeme kwa kupatiwa taarifa ya muda mrefu.
Wengi
wetu tunaunga mkono mipango ya Tanesco ya kuboresha huduma za umeme nchini
ikiwamo kuwakumbuka wananchi wa vijijini kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (Rea),
lakini
Kitu
cha muhimu na cha msingi ni kwamba Watanzania wanapaswa kujengewa mazingira ya
kusahau kero za nishati ya umeme hususani mgawo uliowatesa kwa nyingi.
Kwa
kuanzia kuna haja kwa shirika kuanzia utaratibu wa kutoa taarifa mapema kwa
umma kuhusiana na kuwapo kwa mgawo wa umeme pale kutakapokuwapo na matengenezo
au kuunganisha bomba la gezi katika Grid ya Taifa, ambayo ni tegemeo la maeneo
mengi ya nchi kupata umeme.
Watanzania
kwa muda mrefu walibeba mzigo wa umeme kiasi kwamba nishati hiyo imegeuka kuwa
huduma ya upendeleo kwa walio wengi badala ya kuwa ya lazima kwao.
IMETUMIKA: TAIFA LETU
=======
=======
COMMENTS