$type=slider$snippet=hide$cate=0

Mgombea ubunge CUF aitisha CCM

Na Mwandishi Wetu, Kilwa MBUNGE wa jimbo la Kilwa Kusini anayemaliza muda wake, Seleman Bungara, amesema safari hii atamshinda kwa ...



Na Mwandishi Wetu, Kilwa
MBUNGE wa jimbo la Kilwa Kusini anayemaliza muda wake, Seleman Bungara, amesema safari hii atamshinda kwa kura za kishindo mgombea mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Hasnain Dewji aliyeshinda kura za maoni ndani ya chama hicho tawala.

Mgombea huyo maarufu kama Bwege aliyesimama kwa mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amesema ushindi huo utachagizwa zaidi ya Ukawa ambapo mwaka 2010 alipata kura 14,610 dhidi ya aliyekuwa mgombea wa CCM wakati huo, Ramadhan Madabida aliyepata kura 14,028.
Madabida ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam alipata nafasi ya kugombea 2010 baada ya kumshinda Dewji katika kura za maoni baada ya kuongoza jimbo hili mwa msimu mmoja wa mwaka 2005 hadi 2010.
Akizungumza na SEMA Usikike jana, Bwege amesema amefarijika mno kuona CCM imemteua Dewji kupambana naye Oktoba 25 na kwamba atamshinda kirahisi tena kwa kura nyingi kwa sababu uchaguzi wa mwaka huu utatawaliwa zaidi na nguvu ya Ukawa.
"CCM kumteua Dewji ni kama vile inatapatapa, haiwezekani aonekane hafai mwaka 2010 na wakamtosa katika kura za maoni halafu leo aje kuwa lulu kwao, wananchi wa Kilwa wataonyesha ukomavu wao kisiasa katika hiki kwa kumkataa Dewji aliyetumwa na CCM," alisema.
 Alisema anajua fika kuwa, Dewji atajaribu kufurukuta ili kusaka ushindi, lakini nguvu ya Ukawa itamshughulikia ipasavyo na kusisitiza kuwa labda CCM ingemrudisha tena Madabida angesumbua kidogo.
Dewji mwenyewe hakupatikana kuzungumzia alivyojipanga baada ya kampeni kuanza rasmi jana kote nchini, ingawa habari kutoka ofisi za CCM wilaya ya Kilwa zinasema, mkakati uliowekwa mwaka huu hautampa nafasi Bwege kutetea kiti chake.
Mbali na Bwege na Madabida vyama vingine vilivyogombea ubunge jimbo la Kilwa Kusini mwaka 2010 ni Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kilichopata kura 287, NRA (91), NLD kura 79.

COMMENTS

Name

HABARI,17,MAKALA,2,UCHAMBUZI,2,
ltr
item
TTAJA KIJIJI BLOG: Mgombea ubunge CUF aitisha CCM
Mgombea ubunge CUF aitisha CCM
TTAJA KIJIJI BLOG
http://ttajakijiji.blogspot.com/2015/08/mgombea-ubunge-cuf-aitisha-ccm.html
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/
http://ttajakijiji.blogspot.com/2015/08/mgombea-ubunge-cuf-aitisha-ccm.html
true
5988661810178760650
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy