CCM yamtaka asikubali kurubuniwa Yamuahidi Ukuu wa Wilaya akishindwa MGOMBEA ubunge wa Chama Cha Mapinduzi (...
CCM yamtaka asikubali
kurubuniwa
Yamuahidi Ukuu wa Wilaya
akishindwa
MGOMBEA ubunge wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) jimbo la Monduli, mkoani Arusha, Namelock Sokoine, amejikuta
akiangua kilio mbele ya mgombea urais
kupitia Chadema Edward Lowassa baada ya mwanasiasa
huyo anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Ukawa kumtamkia kuwa hamuungi mkono tena.
Namelock ambaye ni mtoto wa
Waziri Mkuu wa zamani Edward Sokoine,
yupo kwenye harakati za kutaka kumrithi Lowassa aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa
muda mrefu.
Kutokana na Lowassa kuwa mgombea
imara na mzito katika Jimbo la Monduli,
Namelock alitegemea angepata sapoti kubwa toka kwake hali ambayo imekuwa
kinyume.
Tukio la kuangua kilio lilitokea
mjini, Babati katika kikao cha ndani ambacho kiliwakutanisha wagombea wa Chadema
katika jimbo hilo pamoja na mgombea wa CCM,Namelock, akiwa na familia
yake.
Kikao hicho kiliitishwa
na Lowassa baada ya kuwepo na taarifa za
kizushi na za kipropaganda zilizodai kuwa Namelock bado anaungwa mkono na Lowassa
Ikumbukwe kuwa wakati Lowassa akiwa katika harakati za kutaka urais kupitia
CCM, Namelock alikuwa ‘mtu wake’.
Katika tukio hilo Lowassa
alianza kuzisikiliza pande mbili ambazo zilizokuwa zikisigana kuhusu nani hasa
anastahili kuungwa mkono kuwa mbunge wa jimbo la Monduli.
Katika Jimbo hilo Chadema
kimemsimamisha, Julias Kalanga huku CCM wakimsimamisha Namelock.
Awali Namelock alilalamika
hatua ya yeye kutukanwa na kuzalilishwa na mgombea wa viti maalum wa jimbo hilo
(Chadema) Cesilia Ndosi.
Alimweleza Lowassa
kuwa Cesy amekua akimwambia kuwa hajasoma na wala hajawahi kuwa na
cheo chochote shuleni hivyo ni dhaifu hafai kuwa mbunge katika jimbo la Monduli
Kwa upande wake Cesy
alimweleza Lowassa kuwa ni kweli maneno hayo amekuwa akiyasema jukwaani kwa
kuwaeleza wananchi kuwa mgombea huyo hana elimu, kwani alisoma naye sekondari na hawezi kuwaongoza
wananchi wa Monduli.
Hata hivyo alimtaka Lowassa
awaeleze kinaga ubaga ni nani anafaa kuwa mbunge wa Jimbo hilo.
Baada ya ombi hilo ndipo Lowassa
alipotamka wazi kwa kumweleza Namelock kuwa alimpenda awe mrithi wake katika jimbo
hilo wakati akiwa CCM lakini wakati huu amempenda zaidi Kalanga wa Chadema,
baada ya kujiengua kwenye Chama hicho kinachotawala.
Lowassa alimshauri Namelock
aachane na ubunge katika jimbo hilo na amfuate Chadema na hatimaye Ukawa hatua
ambayo ilimfanya Namelock aangue kilio.
Binti huyo aliendelea
kuangua kilio zaidi pale Lowassa alipomshika mkono Kalanga na kuwaambia watu
“Jamani huyu ndiye mwanangu mpendwa ninayependezwa naye, mpeni kura.”
Hata hivyo habari toka CCM
zinasema kuwa CCM iliunda timu ya watu wazito kwenda Monduli kumshawishi
Namelock asikubali kuhama CCM kwa madai kuwa hata akishindwa atapewa hata Ukuu
wa Wilaya.
Imeelezwa kwamba timu hiyo
ilipitia pia kwa wazazi wa Namelock kwa lengo la kumtisha binti huyo.
CHANZO: TAIFA LETU
COMMENTS